Kutana na mwanadada ambaye anaendesha maisha yake kwa kazi mbalimbali zikiwemo uigizaji, muziki, uanamitindo, ujasiriamali na utangazaji.
Miss Tanzania namba 2, 2006, Jokate Mwegelo akipozi.
Huyu ni Jokate Mwegelo ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006. Wiki hii yuko hapa kujibu maswali 10 ambayo mwandishi wetu alimuuliza na akatoa ushirikiano katika kuyajibu.
Ijumaa: Kuna madai kwamba sasa hivi unatoka kimapenzi na mtangazaji wa Clouds, Millard Ayo, hili unalizungumziaje?
Jokate: Hahaaa, kiukweli nampenda sana Millard na ninachompendea ni vile anavyojituma.
Ijumaa: Hujaweka wazi, ni kwamba unampenda kama mpenzi wako au unampenda tu lakini siyo wako?
Jokate: Sijapata mchumba, bado natafuta ila yeye nampenda tu kwa vile anavyojituma.
Ijumaa: Ukiwa chumbani unapenda kuvaa mavazi gani?
Jokate: Mimi napenda kukaa kama nilivyozaliwa.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe.
Ijumaa: Ni kitu gani kinachoweza kukugombanisha au kukuachanisha na mpenzi wako?
Jokate: Kwa kweli nikigundua ana mtu mwingine hapo lazima pachimbike.Ijumaa: Warembo wengi huwa hawajui kupika, wao ni chipsi kuku au chipsi mayai, kwako hili likoje?
Jokate: Napenda sana kupika tena kwenye pishi la pilau mimi ni mtalaam ile mbaya.
Ijumaa: Unaonekana unafanya kazi nyingi sana kwa wakati mmoja, unawezaje kujipanga?
Jokate: Kila fani nimeitengea muda wake na siku zake ndiyo maana kila kitu kinakwenda vizuri na kwa ufanisi.
Ijumaa: Hebu tupe siri ya urembo wako.
Jokate: Niwapo nyumbani napenda sana kufanya mazoezi lakini pia nimejiwekea utaratibu mzuri wa kula.
Mzee wa 'The Count Down', Millard Ayo akipozi.
Ijumaa: Kwa mfano leo hii ukiwa kiongozi wa nchi hii ni mambo gani utayapa kipaumbele?
Jokate: Yapo mengi ya kufanya lakini kwanza nitaboresha
sekta ya elimu na afya kwa sababu ni mambo yanayochangia sana maendeleo ya nchi.
Ijumaa: Ni kiongozi gani ambaye anakuvutia utendaji kazi wake?
Jokate: Nampenda sana January Makamba kwa kuwa ana maneno mengi lakini ni ‘smart’. Ana mipango mingi na anafaa kuwa rais 2015. Pia nafurahishwa na Zitto kwa kuwa ni sauti ya watu.
Ijumaa: Unafikiria kujiingiza kwenye siasa?
Mhe. Januari Makamba akizungumza jambo.
Jokate Sijui ila huenda ikawa hivyo maana napenda sana kuwatumikia watu.
Ijumaa: Mwisho, toa neno kwa Watanzania walio nyuma yako.
Jokate: Nawaomba waendelee kusapoti kazi zangu, nawapenda na nawaheshimu sana kwani bila wao mimi si lolote katika fani zinazonifanya niendeshe maisha yangu vizuri. Nawashukuru sana.
Chanzo:Gazeti la Ijumaa
No comments:
Post a Comment