Monday, 8 December 2014

CRISTIANO RONALDO AVUNJA REKODI YA HAT TRICKTRICK LA LIGA

Kocha wa Real Madrid, Muitaliano Carlo Ancelotti ameelezea uwepo wa Cristiano Ronaldo’s katika kikosi chake kama faida baada ya nyota huyo kufunga goli tatu peke yake (Hat-trick) na kufikisha jumla ya goli 200 katika kigi hiyo wakati madrid ilipoishindilia Celta Vigo 3-0.Katika pambano hilo, nyota huyo toka ureno, Cristiano Ronaldo alifunga goli zote tatu na hivyo kuvunja rekod ya hattrick ya la liga akifikisha 23, moja zaidi ya Magwiji Alfred Di Stefano na Telmo Zarra, huku zikiwa tatu zaidi ya mpinzani wake wa karibu Lionel Messi mwenye 20. Ikumbukwe nyota huyo sasa amefikisha jumla ya goli 200 katika michezo 178 pekee ya La Liga aliyoshiriki ikiwa ni kasi zaidi ya nyota yeyote.


Katika mechi hiyo nyota huyo aliaanza kufunga kwa penati kufuatia kuvutwa eneo la hatari kunako kipindi cha kwanza na hivyo kutokufanya ajizi kuujaza mpira huo kimiani, kabla hajaongeza la pili na la 3 kipindi cha pili akimalizia krosi ya nota kukota Brazil, Marcelo.

Mpaka sasa nota huyo amefunga jumla ya magoli 23 katika michezo 24 ya la liga msimu huu huku ushindi wa jana ukiiwzesha miamba hiyo (Real Madrid) kuwafikia wapinzani wao Barcelona kwa kuishinda Celta vigo mara 18 mfululizo rekodi iliyowekwa chini ya mholanzi Frank Rijkaard msimu wa 2005-06. Klabu hiyo inaivaa timu toka ubeeligiji Ludogoretz jumanne na kama itashinda itakuwa imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya kihispania kushinda mfululizo katika michuano mbalimbali

No comments: