Thursday, 11 December 2014

Dk.REGINALD MENGI AAMUA KUTANGAZA TAARIFA YA HABARI MWENYEWE KISA UHABA WA WATANGAZAJI WASOMI...

Unaweza ukashangaa na kustaajabu huku ukijiuliza maswali kibao.....Hii ni hali halisi wala si udaku au habari ya uzushi.....Shuka nayo upate kisa na mkasa cha mzee kuingia studio mwenyeweeeeeeeeeeeee.........


Mwenyekiti mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi mwaka 1994 alishawahi kuwa mmoja wa watangazaji wa kituo cha televisheni cha ITV wakati huo ndio kinaanzishwa. na kinaanza. Dk.Reginald Mengi alikuwa akisoma taarifa ya habari ya saa 2usiku, ambayo ilikuwa ikionekana kwa njia ya video ambazo hazikuwa na ubora mzuri kimwonekano ukilinganisha na hivi sasa. 


Sasa hivi Dk.Reginald Mengi amekuwa si msoma habari tena kituoni hapo, bali amekuwa ndie mmiliki wa ITV ambayo iko chini ya kampuni yake mwenyewe ya IPP Media inamiliki vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini kama vile Redio One, East Afrika Redio na Tv, Capital Redio na Tv na Magazeti ya The Guardian, Nipashe, Lete Raha, Taifa Letu na Alasiri.
Wakati kituo cha ITV kinaanza kurusha matangazo yake rasmi ya televisheni mwaka 1994, hakikuwaHakim jaw na watangazaji wengi kwani wasomi wenye taaluma ya utangazaji hawakuwepo kwa wakati huo, ndio maana Dk. Reginald Mengi alijitoa kama mmiliki kwa kituo kicho kuwa mmoja wa watangazaji ili kuziba moja ya pengo la watangazaji wachache waliokuwepo kituoni hapo.Hata hivyo haikuwa rahisi kupata watu wenye taaluma na uwezo wa kutangaza katika televisheni ndio mana mmliki huyo alionelea aanze na yeye mwenyewe akiwemo kama mmoja wa watangazaji.
Leo hii kituo cha ITV ndio kituo kikubwa hapa nchini Tanzania kilichoajiri watangazaji wengi wasiopungua 50 wote wenye taaluma kubwa na nzuri ya utangazaji. ITV imekuwa televisheni ya kwanza nchini kuchukua tuzo ya SUPERBRAND Mwezi Februari mwaka 2013 kutokana na ubora wake wa matangazo na vipindi vizuri vinavyoielimisha na kuburudisha jamii yote kwa ujumla hapa nchini na hata nje ya nchi kwa wale wanaowapata kwa njia ya Satelaiti.
Mmiliki huyo wa kituo cha ITV kwasasa ni mmoja wa watu matajiri sana hapa nchini kwa umiliki wake wa vituo hivyo vya utangazaji pia kumiliki vitu vingine mbalimbali tofauti na IPP MEDIA ambavyo vyote hvyo vinavyomuingizia kipato kikubwa sana.

HAKIKA TUMETOKA MBALI....HONGERA ITV NA REDIO ONE KWA KUTIMIZA MIAKA 20....

No comments: