Thursday, 11 December 2014

HUYU NDIYE MSANII WA BONGO MOVIE MWENYE WATOTO WENGI KULIKO WOTE.....ANA WATOTO 8...



MWONGOZAJI na mwigizaji mahiri katika tasnia ya filamu za Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, ametaja idadi ya watoto wake akisema wapo wanane tu. Amekanusha vikali kuwa na timu ya mpira (watoto 11) idadi inayovumishwa na wengi.
Dude anatajwa kuwa ni msanii anayeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto kwa wasanii wengine wa kiume wa Tanzania. 
“Kila mtu anasema anavyojisikia, mara ooh Dude ana timu nzima ya mpira wa miguu, lakini ukweli ni kwamba nina watoto wanane tu, ambao nimezaa na wanawake wanne,” alisema.
“Kwangu naona si haba maana kuna watu ambao hatujui kama wana majukumu, kila siku wanajiona watoto wanayakimbia majukumu yao, mimi sipo hivyo.”
Dude aliongeza kuwa anawapenda watoto wake na ndio maana kila mmoja wao alipozaliwa na kubainika ni wake, alianza mara moja kutoa huduma na kumtambulisha kwa familia yake.
“Unajua wapo wasanii wengi tu wenye watoto, lakini wengine hukimbia majukumu kwani wanataka wanataka kila siku kula starehe na mizigo kuwaachia waliozaa nao,” aliongeza.

No comments: