Sunday 7 December 2014

SFW YAWAKUTANISHA WEMA,DIAMOND NA MOHAMED DEWJI



Mwanamuziki nyota wa miondoko ya Bongo Fleva nchini, Nasib Abdul, ‘Diamond Platinum’ anashindana na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu katika kuwania Tuzo ya Mtu mwenye ushawishi mkubwa katika mitindo.
Tuzo hiyo zitatolewa kwenye Onyesho la Mavazi la Swahili Fashion 2014 linaloandaliwa na Kampuni ya 361 Degrees, Desemba 7.
Katika shindano hilo lililoanza jana wengine wanaoshindana ni pamoja na Mwamvita Makamba ambaye namba yake ya kupigiwa kura ni SFW SY 01, Millen Magesse(SFW SY 03) na Mohamed Dewji SFW SY 04
Katika mpambano huo Diamond atapigiwa kura kupitia namba SFW SY 02, huku Wema Sepetu ikitumika namba SFW SY 05.
Diamond pia anashindana katika kipengele cha Wanaume Wenye Kuongoza, huku namba yake ya ushiriki ikiwa ni SFW SMP 01 akichuana na Luca Neghesti(SFW SMP 01), Baraka Shelukindo(SFW SMP 03), Noel Ndale(SFW SMP), Rio Paul(SFW SMP 05) na Juma Juxx mwenye nambari SFW SMP 06
Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa tuzo hizo, Haruna Ibrahim alisema kuwa kwa mwaka huu kuna ushindani mkubwa katika kila kipengele.
Aliongeza kuwa Martin Kadinda naye anawania tuzo katika kipengele cha Mbunifu Bora wa mchango katika tasnia hiyo ambapo anashindana na kina PSJ Couture(SFW MWD 01) huku yeye akiwa na nambari SFW MWD 02. Wengije ni Mtani Nyamakababi(SFW MWD 03), Manju Mitta(SFW MD 04) na Gabriel Mollel(FW MWD 05)
Ibrahim aliongeza kuwa kwenye kipengele cha Mbunifu wa Mavazi Bora wa mwaka wanaoshindania Kadinda, Gabriel Mollel, An Nisa Abayas na Eve Collections.
Alisema kuwa kwa upande wa Baileys, Mwanamitindo Bora wa Kike kwa mwaka huu, wanaoshindana ni Jamilla Nyangassa (SFW FM 01), Gyver Meena(SFW FM 02), Jihan Dimachk(SFW FM 03), Neema Kilango(SFW FM 04), Joceline Maro(SFW FM 05) na Lethina Christopher(SFW FM 06).
Kwa upande wa wanamitindo bora wa kiume wanaoshindania tuzo hizo ni pamoja na Danny David (SFW MM 01), Victor Casmir(SFW MM 02), Dietrich Luhanga(SFW MM 03), Ally Daxx (SFW MM 04).
Haruna alifafanua kuwa kwa upande wa Tuzo za Mwanamitido Bora wa mwaka kwa Afrika Mashariki wanaoshindaniwa ni pamoja na Vivian Mutesi (SFW EAM) na Sharon Mirembe Sanya (SFW EAM 02) wote wa Uganda, Christina Masese (SFW EAM 03) na Ajuma Nasenyana (SFW EAM 04) wote wa Kenya.
Kwa upande wa Tuzo ya Mbunifu wa mwaka aliwataja wanaoshindana na namba zao kwenye mabano kuwa ni pamoja na Kiki’s Fashion(SFW DY 01), Jamilla Vera Swai, (SFW DY 02), Ailinda Sawe(SFW DY 03), An Nisa Abayas ( SFW DY 04), Manju Msita(SFW DY 05) na Lucky Creations( SFW DY 06)
Katika mashindano hayo pia itatolewa tuzo ya mwaka kwa mtaalamu wa urembo na nywele huku wanaoshindaniwa wakiwa pamoja na Rehema Samo(SFW HMA 01), Asila Makeup(SFW HMA 02), Glambox(SFW HMA 03), Lavie Makeup Studio(SFW HMA 04)
Wanaoshiriki katika kipengele cha kushindani tuzo ya vidani ni The Mabinti Center (SFW AD 01), Enjipai Jewelleries(SFW AD 02), Florinyah Designs(SFW AD 03), Sairiamu(SFW AD 04), Linda August(SFW AD 05) na Nyumbani Designs(SFW AD 06)
Watakaoshindania tuzo katika kipengele cha mbunifu wa Afrika Mashariki ni pamoja na Martha Jabo (Uganda), SFW EAD 0, Afrostreet Kollektions (Kenya), SFW EAD 02, Arapapa by Santa Anzo (Uganda), SFW EAD 03, Akinyi Odongo (Kenya), SFW EAD, Kiko Romeo (Kenya), SFW EAD 05 na Mille Colliness (Rwanda), SFW EAD 06.

No comments: