Saturday 29 November 2014

SAKATA LA ESCROW,HATIMAYE WASIRA ATOA MATAMKO MAKALI..



Wasira: CAG sio mara ya kwanza kuchunguza na kuleta taarifa bungeni, na PAC nao hii ni kazi yao kuchunguza na kuleta Bungeni

Wasira: Jambo la pili ni wajibu sasa wa Bunge hili kutazama ripoti hizi na kuzifanyia kazi.
Wasira: Kama kuna mtu anataka kuwa Rais na mbinu zake ni kuondoa wengine huyo hafai kabisa kuwa Rais wa Tanzania

Wasira: Sisi bunge hili lazima tunangalie maslahi ya Watanzania, hatuwezi kutumiwa na mtu.
Wasira: Afadhali kuwa maskini mwenye heshima kuliko tajiri anayetukanwa
Wasira: Tutakuwa Bunge la ajabu kama maneno haya yameandikwa na vyombo hivi vya Bunge halafu sisi tukalifumbia macho.

Wasira: Nchi ambayo unaenda na sandarusi, mabox kubeba hela, hapa hatuna nchi, inabidi TAKUKURU watutajie ni kina nani hawa

Wasira: TAKUKURU iwachambue watu wote bila kujali vyama au nini ili tuwapeleke kwenye sheria
Mwandosya: Suala hili linatuondolea sifa kama nchi, linatuondolea heshima kama taifa, kimataifa na mbele za wananchi

No comments: