Saturday 29 November 2014

MJADALA MZIMA WA SAKATA LA ESCROW NA MAAZIMIO YALIYOFIKIWA KATIKA VIKAO VYA JANA MCHANA NA JIONI..


MJADALA

Nchambi: Anailaumu serikali kwa kuchelewesha kuleta jambo husika bungeni, watanzania wana hamu ya kujua fedha ni nani? Wakili wa TANESCO(Mkono) alishauri kufunguliwa akaunti(ananukuu maandiko ya biblia kuhusu kuheshimu mamlaka), anasema kila mtu atawajibika kwa namna yake.


Hasara nyingine tuliyoipta ni gharama za mawakili(bilioni 62) ambayo watuwengi hawaigusii, kesi imeenda miaka kumi hivyo haki kupatika ilionekana ni ngumi na bado tunadaiwa. Baada ya malipo tutakuwa tumepoteza bilioni 90 kwenye kesi.

Lazima tuangalie pande zote mbili, sehemu serikali inapotakiwa kuwajibika pia watu binafsi watatakiwa kuwajibika, fedha baada ya kutoka escrow na maamuzi(ruling) kutoka. Ilionekana bado TANESCO bado ingedaiwa lakini lazima serikali ituletee majibu dhidi ya mgogoro wa capacity charges.

Wizara ya nishati na madini ilikuwa na matatizo mengi kabla ya Prof Muhongo, tunapojadili hoja tujadili yenye mashiko. Tanzania ina kata 3804, Muhongo ameingia katika bajeti moja na kusambaza umeme vijiji vingi (ananukuu Quraan kuhusu kusema kweli).

Ananukuu Biblia watu wasiwe wakorofi(kumuingilia wakati anaongea), fedha za Escrow sio ugomvi ya ubadhilifu wa fedha pekee. Bei ya umeme tunaouziwa imeshika baada ya Muhongo, anasema kunaweza kuwa na chuki ya kibiashara hivyo tutumike kwa masilahi ya nchi na sio wafanyabiashara. 

Kuwatisha wawekezaji sio jambo jema na tutapoteza imani na wawekezaji, waliotajwa kuhusika na fedha hizo serikali iwachunguze. Wapo watu wameingiziwa fedha kwenye akauti zao. Ananukuu Quraan kuhusu haki na batili, anapata mashaka mbunge kwenda kukagua wakati yeye pia anatiliwa mashaka. Kuna list ya watu itakuja hapa bungeni, kuna watu wa kambi ya pili wametetea hili jambo kwa upole na unyonge. Wabunge tusimamie haki na tuseme ya kweli, tulianza na Mungu na tuendelee na Mungu. Anamsifu Muhongo kwa kazi anayoifanya wizarani. Waziri mkuu ametajwa, ametajwa kwa namna tofauti na kuna watu ni majeruhi. Ananukuu Quraan kuhusu wajuzi, niwatie moyo mjadala uende vizuri.

Mwigulu Nchemba: Ukububwa wa jambo tunaongelea maadili na maslahi ya watanzania, nitajikita eneo linalogusa wizara ya fedha. Nazipongeza taasisi zote zilizoshiriki kwenye ripoti hii(anazitaja). Tangu utaratibu huu uanze, chimbuko la ripoti hii ni serikali yenyewe.

Kodi, imegawanyika maeneo matatu, VAT haikukatwa na kukatokea mkanganyiko, TRA inashughulikia na ni ilikua ni bilioni 26.97 lakini baada ya kugundua kuna kodi ya wananchi haijakusanywa ndipo wakakusanya bilioni 4.1 na ukaguzwa ni wa kwenye Escrow na sio IPT. Niwahakikishie watanzania kuwa kodi hii italipwa, hatuwezi kuacha kodi kwa tajiri halafu tukimbizane na mama mjane anaeuza mchicha barabarani.

Kodi ya pili ni iliyotokana na kukosewa kwa mahesabu na ni lazima ilipwe, TRA imeshaandika barua ya Novemba 2014 ya kufuta cheti(certificate). Brela wameshapewa notice ya kufuta capital gain certificate iliyotolewa kipindi kilichopita. Hatua imechukuliwa na serikali na tuko makini. Kuna watu wasio waaminifu, kuna mtu badala ya kuandika $ milioni 6 akaandika Tshs milioni 6 na badala ya kuandika $milioni 20 ameandika Tshs 20. Naagiza mamlaka ya TRA ifanye uwajibishaji wa ndani na akafanye kazi nyingi na hakuna uchunguzi juu ya uchunguzi. Mtu aliyeiba ukimfukuza kazi ni kumpa likizo akatumie fedha alizoiba hivyo mamlaka husika wachukue hatua. Tumeambiwa kuhusu pesa zilizogawiwa, na wenyewe walipie kodi kabla ya tarehe 31/12/2014. Baada ya tarehe hio TRA wafatilieni mmoja mmoja. Kuna taarifa pesa zilitoka kwenye mafurushi na magunia, nimefatilia na wamefata sheria. Anatoa agizo kwa Stanbic na Mkombozi watoe matamko, wateja wao wana haki ya kujua reputation ya benki yao. Niwaombe wabunge, kuna kuongea na kuchukua hatua na watanzania wanasubiri kuchukua hatua. Tumekua tunawachukulia hatua wanasiasa lakini wataalamu waliosomeshwa kwa kodi hawajibiki popote.(Muda umeisha)


Kafulila: Benki ya stanbic wamemfukuza kazi aliefungua akauti ya PAP amefukuzwa kazi asharudi kwao Uganda hivyo hizi ni dalili kuwa kuna makosa yalifanyika ndo maana hatua zimechukuliwa.

Mnyaa: Nampongeza Nchemba kwa kusimama katika ukweli, economic hitman ni kama Mafia, na washawahi kuziangusha nchi(anazitaji) na miradi mikubwa wanayohusika nayo ni kama ya umeme, tujiulize kama hawajaingia Tanzania. Nyaraka nyingi zilizothibitishwa akatoa mbunge kuzikanusha ni kosa, Muhongo anasema ana nyaraka muhimu kwannini hakuzipeleka kwa CAG, maadili ya viongozi ambayo katika maazimio ya Richmond yaliazimiwa. Mwanasheria wa RITA leo yupo katika IPTL na mgao. CAG anapinga wabunge kuwa wajumbe wa bodi, leo hii sio conflict of interest? Wahusika ni IPTL na TANESCO na BoT NI MSIMAMIZI.

Imekuwaje BOT kutuma pesa PAP badala ya IPTL, kwa nini imekiuka akouti ya Escrow.

Mchangiaji: Ni dhambi kudhania PAC ni chombo cha wapinzani, kama kuna mapungufu ni bora tuyarekebishe, wanaofanya haya wanakula na viongozi wetu wa juu. Katika hili wananchi wameathirika sana kutokana na balaa hili la overcharge. Haiwezekana watu kuchukua pesa za dhulma na sisi wanyonge kuzilipa. Hakuna yoyote aliye alie juu ya sheria, uwajibikaji ni la lazima. Mbona alijiuzulu kwa mzigo wa watu wengine kwakuwa walikuwa chini yake.

Ashumta Mshana: Kuna taarifa tatu, ya serikali, PAC na CAG ila ukisoma zote zimetofautiana hivyo kutufanya tusielewe vizuri, taarifa ya PAC ina mapungufu mengi. Mbowe ametajwa kupokea pesa lakini haijataja.

Taarifa: PAC inafanyia kazi taarifa ya CAG, hayo majina unayoyasema hayakuwepo.

Ashumta: Kwani mapendekezo ya PAC yapo kwenye taarifa ya CAG

Mwenyekiti: Si vizuri kutaja majina ambayo hayapo kwenye ripoti.

Ashumta: Benki ya Mkombozi pekee majina yake ndio yameletwa, tunataka na majina ya Stanbic. Waziri mkuu hawezi kuondoka, tunao uhakika mbele yetu. Ripoti ya CAG hakukuwepo kuwa Muhongo amehusika moja kwa moja.

Waziri wa nchi: Kwa mujibu wa kanuni, nasogeza muda wa bunge mpaka saa nane mchana.

Nkumba: Serikali lazima ichukue hatua, haiwezakini ukapewa bilioni na Lugemalila lazima aseme alitoa hizo fedha kwa ajili ya nini. Nimshukuru Lugemarira ametusaidia sana kumaliza hili jambo hili. Hata kama ni chama cha mapinduzi tuwashughulikie.

Sendeka: Hapa hamna uwajibikaji wa pamoja bali mtaje wahalifu, wahalifu lazima wabebe, hakuna majina ya watu kwenye mauzo, huhitaji akili kubwa kujua kuwa hapa kuna uhalifu, watu wamekwepa kodi bilioni 8.7 kwa watu kughushi, haihitaji upoteze muda, utajua hapa kuna utapeli tangu mwanzo, kusimama na kusema ofisi ya CAG ni uongo mtaiambia nini dunia kwamba vyombo vyetu vyetu tulivyoviweka ni uongo. Hii ni dhambi, watu wanaopata fadhila za wizara wanakaa kwenye kamati. Muhongo kafanya kazi ya udalali, watanzania ni vyema wakapata majibu kama ni kweli ama la, kwenye mkataba unamtaja mheshimiwa Muhongo(anaunukuu)

Muhongo anaomba taarifa kuwa anachosema Sendeka ni uongo na kilichoandikwa si lazima awe sahihi, niwahakikishie watanzania hakuna mwekezaji yeyote nchi hii ambae hajaja kuonana na mimi.

Zitto: Nyaraka za CAG zimekua verified lakini za Muhongo alizozitoa uongo, mkataba unasema walikutanishwa na Sendeka.

Sendeka: Nimesoma kwenye mkataba ambao pia uko ofisini kwako na wewe umeshiriki, profesa aliita nyaraka nilizozileta ni za kufungia maandazi, hakuna shaka kuwa Muhonga alikua dalali katika dili hili, nina uhakika miongoni walionufaika ni waliowezesha dili hili. Ingekuwa haunizidi umri ningesema ulichofanya ni ukuwadi. Kodi la ungezeko la mtaji kila mmoja anajua tulivyoibiwa, ushauri wa nwanasheria mkuu umekwepesha kodi nchi hii, tunamlinda kwa sababu gani, Muhongo na Maswi pia bodi ya TANESCO inabaki kwa sababu gani! Tulimwajibisha, waziri leo anapewa masaa mawili kuitetea serikali ambayo si ya serikali bali wake mwenyewe. Mlienda Kunduchi kugawana fedha kwa njaa. Isaidieni nchi hii, hamuwezi kukwepa kodi alafu mkaja kutetea. Mwisho tupige kura juu ya mambo haya. Hatujakokotoa na bado tukampa Lugemalira 
lakini alilipa mabilioni ya kodi wakatiSeth mmemuacha. Mkono mlimpa dili wenyewe na mwanasheria wa TANESCO mkamfukuza bila haya, mi naomba waziri mkuu arudishwe. Huitaji kuwa msomi kujua. (Muda umeisha)


Lekule: Mhe M/Kiti, Hili suala tusiliwekee utani. Tusilizungumze wala kulijadili kwa mzaha. Ni jambo zito tusilete siasa. Sio suala la CCM kuiba fedha za UKAWA wala kinyume chake bali ni suala la wizi wa fedha za Umma.

Kiwango cha fedha kilichoibiwa, ni kiasi kikubwa. Hatuwezi kusema hizi pesa sio za umma, maana kuna fedha za kodi, hata kama pesa ni za mashirika, lakini zina kodi ndani yake. Kwahiyo ni fedha za Umma kwa na namna moja ama nyingine.

Akaunti ya escrow imeingiliwa na wezi wa aina mbalimbali. Leo tutafute sumu ya kuwapa hawa wezi wa hizi fedha.

Mhe. M/kiti, haya mabilioni yaliyogawanywa utashangaa, hivi huyu tajiri aliyegawa hizi fedha,anataka nini kwa hawa watu wote hawa? Hata duniani kote haijawahi kutokea tajiri akagawa pesa kwa namna hii. 

Hizi fedha ni za jasho lake kweli? Maana haitegemewi fedha za jasho lake kugawiwa kwa namna hii, Matarajio yake ni nini kutoka kwa hawa watu?

Mhe. M/kiti, TANESCO ni shirika la umma, kwahiyo kama kuna fedha za TANESCO humo ndani tuna haki ya kudai. Kama ikishindikana kutowawajibisha hawa waliohusika na wizi huu, basi ni bora waliotangulia kama wakina lowassa, ngeleja na wengineo waje tuwaombe radhi, Kwa sababu sioni tofauti ya hawa viongozi.

Kwa sababu sitegemi nipewe 1.6 bilioni bila kujiuliza, hizi fedha ni za nini? 

Kwahiyo naomba uchunguzi ufanyike zaid. Mimi nawapongeza kamati ya PAC, wamefanya kazi nzurri na bunge tuige kamati hiyo. Naomba na kamati nyingine zitakazochaguliwa kufanya kazi kama hii waige mfano huu.

<<<<<<>>>

Lekule: Mhe M/kiti bado nasema, hii kazi tunayofanya tufanye kwa umoja bila kumuonea mtu na tusilindane tufanye kama inavyotakiwa..(Makofi)

Asante sana.

====================

Mwenyekiti wa bunge, Mussa A. Zungu anaahirisha kikao cha bunge hadi saa 10 badala ya saa kumi na moja jioni, ili wachangiaji wawe wengi na kupata muda wa kutosha.

Wachangiaji watakaoanza jioni ni; 

- John Mnyika
- Halima Mdee
- Esther Bulaya.............na wengineo.

Asanteni.
==============


DONDOO MUHIMU KIKAO CHA JIONI

Kigwangalla: Sijawahi kuona Profesa muongo kama Muhongo
Kigwangalla: Toka lini pesa za watu binafsi zikawekwa Benki Kuu?

Mpina: Ni bahati mbaya tuna Profesa muongo kama Muhongo ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini
Mpina: Pesa zilizotolewa hazijalipwa kwa mmiliki halali wa IPTL, PAP sio wamiliki halali!
Mpina: Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliingilia majukumu ya TRA ktk kukusanya kodi

Zitto: Nimekuwa na mgogoro na chama changu lkn kwenye hili wameniunga mkono, kwa mara ya kwanza nimehudhuria kikao cha UKAWA
Zitto: Kuna baadhi ya wajumbe wanadai tumetumwa na Uingereza. Hakuna kinachonituma kufanya haya, ni uzalendo kwa nchi yangu
Zitto: Mahakama ilikiri kuwa kweli tulikuwa overcharged; ikaamriwa yafanywe mahesabu upya!
Zitto: Prof. Muhongo alisema anaheshimu mahakama za ndani. Jaji utamwa hakuwa anaamua kesi ya Escrow wala Capacity Charges
Zitto: Jaji hakusema kokote kuwa toeni hela mkawape IPTL. Hakuna sehemu alikotaja kitu kama hicho
Zitto: Kama TANESCO ina madeni makubwa na haina hela; Tanzania ina deni kiasi gani la Taifa? Basi tumeshauzwa!
Zitto: Muhongo alikuta TANESCO ikiwa na hasara ya Bil 43. Sasa TANESCO ina deni la zaidi mara 4!
Zitto: TRA wamegundua fraud kwamba nyaraka za PAP zilikuwa forged! Nchemba ameonesha ukomavu ktk hili
Zitto: Hivi watanzania tumefikia hatua ya kuukata utanzania kabisakabisa?
Zitto: Prof. Muhongo anadai yeye hahusiki na mambo ya makampuni. Sheria iliyotungwa mwaka 2012 haisemi hivyo!

Umeme umekatika Bungeni, wabunge wanashangilia!

Zitto: Kijana aliyesema Singh ni tapeli ametengenezewa kesi ya mauaji. Alifukuzwa kazi! Naomba apatiwe ulinzi
Zitto: Prof. Tibaijuka aliniandikia mchango wake wa maandishi kuelezea alivyopata fedha; tunawaachua Kamati ya Maadili
Zitto: System ili-collapse wakati wa mchakato wa uha
mishaji wa mabilioni haya


Zitto: Tuhuma zikiachwa bila kufanyiwa uchunguzi watu huziamini. Naomba tuhuma za Lusinde kwangu zifanyiwe uchunguzi
Zitto: Naomba wanaonishughulikia wanishughulikie mimi; mwacheni mamangu apumzike (anatokwa machozi)

Kafulila: Tusiache kujadili kifo cha Waziri Mgimwa kisa mwanae hataki; kuna siku Rais atakufa na mwanae atataka tusichunguze

Chenge: Naomba neno KUFA listumike bali litumike neno KUFARIKI linakuwa na staha kidogo

Pendekezo la Serikali kumkamata Harbinder Singh Sethi kwa money laundering limekataliwa na Serikali hadi kesi iliyopo iishe

Lissu: Sethi akamatwe. Shauri lililopo mahakamani ni shauri la baadae! Akamatwe kwa sababu jinai kubwa imefanyika
Lissu: Pendekezo hili la serikali naomba wabunge wasilikubali; mtu huyu ahukumiwe kwa jinai
Simbachawene anapendekeza Sethi asikamatwe kama ilivyopendelezwa na Serikali; wabunge wanazomea

Mdee: Si ajabu kwa mtu mmoja kuwa na kesi ya jinai na kesi ya madai. Huyu Sethi afunguliwe kesi ya jinai
Halima Mdee: Kilicholetwa na Serikali ni ovyo, kinalinda wezi (kutaka Sethi asikamatwe mara moja)
Pindi Chana: Wa kukamatwa si Sethi peke yake; vyombo vya dola vifanye uchunguzi kwanza kubaini jinai iliyofanywa

Zitto: PCCB na TRA wameshafanya uchunguzi; mnataka vyombo gani vingine vifanye uchunguzi?

Werema: Eneo hili ndo litaleta mgongano mkubwa kati ya Bunge na Mahakama. Kwa sasa ni vigumu kusema "mkamate"

Makinda: Mnaposema akamatwe mnakosea, sisi siyo mahakama, tutafute njia nyingine na tuweke lugha ya kwetu siyo ya mahakama
==================


MAAZIMIO

Pendekezo la kwanza la kumkamata na kumfilisi bwana Seth lina marekebisho ya serikali, naibu waziri wa Sheria anasema haiwezekani

Pendekezo la pili kuhusu Rugemalira, serikali imeweka marekebisho kuhusu uhalali wa pesa za Rugemalira alizogawa


Azimio la TATU limerekebishwa kuwa waliopokea pesa wachunguzwe na kuchukuliwa hatua mahususi kwa mujibu wa sheria

Pendekezo la NNE. Kamati inazitaka mamlaka kuzitangaza benki za Mkombozi na Stanbic kama asasi za utakatishaji fedha
Azimio la 4 limepita kwamba Kamati inazitaka mamlaka husika ikiwemo benki kuu kuchukua hatua dhidi ya benki zote zilizohusika

Azimio la TANO: Serikali ipitie upya mikataba yote ya umeme na kutoa taarifa kabla ya kumalizika kwa Bunge la bajeti lijalo

Azimio la SITA: kuhusu Bodi ya TANESCO kuvunjwa kwa kusababisha pesa kuchotwa na hasara, serikali imekataa, mjadala unaendelea


Kingwangala: Kanuni zetu zinataka mtu yoyote anayetaka mabadiliko ya maazimio lazima awe amekawasilisha kabla

Kafulila: Kwa mujibu wa mkataba wa IPTL, maamuzi ya mwisho yanafanywa na mahakama ya London, bodi walikuwa na maamuzi hayo na haikuwajibika na maamuzi ya mahakama za ndani ya nchi

Majibu: ISCD ilisharidhia injuction ya mahakama ya Tanzania na ikaijulisha standard charted hivyo si sahihi kusema ISCD ina mamlaka ya mwisho, IPTL pia ilipata injuction kwenye mahakama za Tanzania
IPTL sio kampuni ya kimataifa tena bali kampuni ya ndani

Mdee: Bodi ya TANESCO, napendekeza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi vitendo vya jinai na kuchukua hatua kwa bodi ya TANESCO

Mbowe: Kazi yote hii pengine tusingefika hapa kama bodi ingekua makini, bodi ya TANESCO haiwezi kukwepa lawama hii. Bodi ya TANESCO iwajibishwe

Lissu: Maneno ya Mdee yanahusu jinai, ishu ni bodi ya TANESCO, (Anapendekeza bunge livunje bodi ya TANESCO ivunjwe na iundwe upya kuongeze ufanisi.

Shekifu: Tusifike mahala bunge likatoa amri lakini kutekeleza shughuli pia tuna mihimili mitatu, bunge linaishauri tu serikali na bunge haliwezi kuivunja bodi ya TANESCO

Azimio hili ni la bunge hivyo tuepuke kuvunja katiba

Zitto: Bunge linaelekeza kwamba bodi ya TENESCO liundwe upya maana taasisi zote zimeshachunguza kama TAKUKURU na nyinginezo

Maelekezo ya Lissu yanapitishwa na wabunge

Azimio la Saba: Kamati imethibitisha katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini amefanya uzembe pia amesaidia pesa za Escrow akaunti kulipwa kwa asiyestahili, kamati inashauri uteuzi wake utenguliwe mara moja.

Wa
ziri: Maswala yote yatachukuliwa hatua baada ya uchunguzi.



Kafulila: Halina mabadiliko na kama ni uchunguzi umeshafanywa na CAG na TAKUKURU, bunge kama chombo kinachoisamamia serikali libaki na meno yake ya kuisamamia serikali.

Simbachawene: Katibu mkuu ni mtumishi wa umma, na mwenye mamlaka nae ni raisi wa jamhuri hivyo bunge haliwezi.

Nagu: Nakubalianana uzito wa jambo, watendaji wa serikali wanawajibika kweli lakini wana haki zao, mamlaka husika waangalie na wachukue hatua.

Sendeka: Kamati inapendekeza uteuzi utenguliwe na TAKUKURU wamfikisha mahakamani, sisi tumeshauri na watu ambao tuna mamlaka nao ni waziri mkuu na raisi.

Zitto: Taarifa kwa waziri, taarifa hii inaweza kutumiwa na vyombo vya sheria.

Sakaya: Sio ikithibitika kwani kwa taarifa zilizopo imeshabitika

Suzan Lymo: Kwa uchunguzi ambao umeshafanyika, katibu mkuu huyu ana matatizo kwa sababu PAC na CAG ameshaonyesha

Vyombo vya kiuchunguzi viendelee kufanye uchunguzi

Lissu: Bunge litofautishe maswala la kijinai na mendine sio ya kijinai kama kutengua uteuzi. Wapo wanaolindwa na sheria, lakini wapo wanaoserve kwa mamlaka ya raisi hauwezi ukasema wana protection ya kisheria. Tunaomba nipendekeze bunge linaazima na sio kupendekeza.

Zitto anapendekeza katibu mkuu asimamishwe kupisha uchunguzi.

Wasira: Lazima tukubali nchi inaendeshwa na mihimili mitatu, juzi tulipata tatizo la mahakama kuzuia bunge na sisi pia bunge tusiingilie serikali.

Mchangiaji: Uchunguzi utafanyikaje wakati watu wako kazini?

Werema: Mimi ndiye niliyemshauri Katibu Mkuu Maswi kushughulikia fedha, ninambeba hivyo shughulikeni na mimi

Imeshindikana kupita kwa azimio la saba, Spika kaamua waendelee na azimio la nane, watarudi kupiga kura mwishoni.

Azimio la nane: Bunge limemuondoa Naibu Waziri wa Nishati Masele kwenye mapendekezo kwa kuwa hana hatia ya kuadhibiwa

Azimio la tisa: Linajadiliwa kuhusu kutengua uteuzi wa Waziri Prof Muhongo lakini upande wa serikali imekataa

Bunge halina mamlaka ya kumwambia raisi atengue baada ya Lissu kulitaka bunge kutengua uwaziri wa Muhongo.

Mbaruku: Bunge kazi yake ni kushauri na bunge haliwezi kuwa messenger. (Anashauri anavyoona)

Muhongo ameshutumiwa amedanganya bunge lakini hamna popote iliposemwa fedha hizi ni za umma moja kwa moja. Hivyo nashauri versin ya muheshimiwa Chenge.


Shaha: Tunachohitaji ni lugha nzuri bila kudharau muhimili mwingine. Tuhoji na tumalize na tuulize wanaoafiki Lissu au Chenge.

Zitto: Akili yangu imechoka kidogo hivyo sina pendekezo.

Mbowe: Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi.

Baadhi ya wabunge wanasema wezi waondoke...

Sendeka: Naomba tukae na tujenge hoja, (Kelele zinaendelea)

SPIKA ANAAHIRISHA KIKAO CHA BUNGE MPAKA WASHAURIANE TENA(Spika aahirisha kikao cha Bunge ghafla baada ya kutokea sintofahamu baada ya Wapinzani kudai Waziri Muhongo analindwa )




No comments: