Friday 23 January 2015

ZARI KUWA NA MIMBA,INA MAANA DIAMOND ALIFANYA MAPENZI BILA YA KINGA,JE WALIPIMA LINI NA WAMEJUANA KWA MUDA GANI?????


Takribani wiki nzima sasa mitandaoni kumejaa hii habari ya kuwa shemeji na wifi yetu Zari the boss lady yu mjamzito,ambapo muhusika wa ujauzito huo ni Diamond...Nimekuwa nikijiuliza mwenzenu,Ili mtu aweze pata ujauzito kwa njia ya kujamiiana basi ni lazima afanye mapenzi bila kutumia kinga ya aina yoyote ile hususani Condom.. 
Hivyo kama kweli Zari ana mimba hii ina maanisha walifanya mapenzi kavu kavu na hapa ndipo ninapojiuliza mimi mwenzenu ZARI NA DIAMOND WALISHAPIMA AFYA ZAO??? WAMEJUANA KWA MUDA GANI MPAKA WAFIKIE UAMUZI HUO WAKUTEMBEA PEKU PEKU????  

Huko mitandaoni,Shabiki wa Diamond ametuma mtazamo wake kuhusu issue ya Diamond na Zari kutegemea mtoto na kusema.
“Sijawahi kuona mastaa hawa wakiwa hospitalini au kwenye kituo chochote wakipima afya zao, ukizingatia ni watu wakuweka hadharani mambo yao yote basi hata kupima wangeweka instagram au huko twitter “

” Ni vizuri staa kuzaa na staa mwenzake ila Diamond ana muda wa kuwa baba? mahusiano yake mengi ni kiki au drama ambazo hata Kwa Zari tuliyedhani itakuwa tofauti kumbe ni yale yale, mimi ni shabiki tu ila nawatakia kila la heri kwenye familia yao wanayoanzisha ”
Shabiki alimaliza hivyo.Upi mtazamo wa juu comment za huyu shabiki ?

No comments: