Friday, 28 November 2014

UNICEF KUJENGA MAHAKAMA YA WATOTO MKOANI MBEYA


Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto Duniani UNICEF limeahidi kusaidia ujenzi wa Mahakama ya watoto Mbeya kutokana na Mkoa huo kukidhi viwango vya uanzishwaji wa Mahakama hiyo ambapo hii itakuwa ni Mahakama ya pili kwa Tanzania, nyingine ikiwa ni Mahakama ya Kisutu Dar.

Mkoa huo umechaguliwa kutokana na kukidhi vigezo vya kuanzishwa Mahakama hiyo ambavyo ni pamoja na uwepo wa madawati ya jinsia na watoto katika vituo vya Polisi na pia uwepo wa Waendesha mashtaka na Mawakili wa Serikali wanaoshughulikia mashtaka ya watoto.

No comments: