Emerson de Oliveira Neves Roque – mbrazil ambaye ameletwa nchini kuja kufanya majaribio na endapo ikifuzu basi ndio itachukua nafasi ya mbrazil aliyeondoka Jaja.Jana jioni mchezaji huyo huyo aliwasili na leo hii mchezaji huyo ameanza mazoezi mepesi asubuhi katika Uwanja wa shule ya Sekondari Loyola kufuatia kusaifri kwa zaidi ya masaa 11 kutoka jijini Rio de Janeiro.
Kiungo mbarazil Emerson de Oliveira a(wa pili kutoka kulia) akiwa mazoezini leo asubuhi katika uwnaja wa shule ya sekondari Loyola, wengine ni Kizza, Javu na Coutinho
Emerson ameungana na wachezaji wengine wa Young Africans katika mazoezi ya leo asubuhi ikiwa ni siku yake ya kwanza katika ardhi ya Tanzania na kufanya mazoezi mepesi mepesi chini ya kocha msaidizi Leonardo Neiva kuijiweka fit na kutoa uchovu safari.
Kiungo huyo mwenye umbo lililonyumbulika ambae alikuwa akichezea timu ya Bonsucesso FC iliyopo lii daraja la pili nchini Brazi katika jiji la Rio de Janeiro pia msimu uliopita alikua akicheza soka la kulipwa katika nchi ya Poland latika klabu ya Piotrkow Trybunalski FC.
Kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo amesema mchezaji huyo leo alikua na programu ya mazoezi mepesi tu kutokana na uchovu wa safari na kesho anatarajiwa kuendelea na mazoezi na wenzake kulingana na ratiba iliyopo.
Endapo Emerson atafanikiwa kulishawishi benchi la Ufundi kumsajili basi moja kwa moja ataingia makubaliano na klabu ya Young Africans kwa ajili ya kuitumikia kwenye michuano ya kimataifa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanznaia bara.
No comments:
Post a Comment