Saturday, 29 November 2014

HAMISA MOBETO ADAI HATEGEMEI WANAUME ILI AISHI MJINI



Hamisa Hassan Mobeto


Mwanamitindo kiwango Bongo, Hamisa Hassan Mobeto amepangua tuhuma ambayo amekuwa akitupiwa na  watu wanaomuona aking’aa kisha kudai anatumia mgongo wa wanaume tofautitofauti (mabuzi).
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Hamisa alisema amekuwa akisikitishwa na tabia hiyo ya watu kumnanga kwenye mitandao ya kijamii kuwa
anatupia picha nyingi ili kujiuza kwa mabuzi kitu ambacho si cha kweli.
“Kiukweli asiyekujua hakuthamini, nasema hivi kutokana na watu wengi wamekuwa wakinisema vibaya hasa katika mitandao ya kijamii, wanikome kwani kila mtu ana maisha yake na mimi sitegemei mabuzi kuishi mjini, nina mpenzi wangu mmoja tu,” alisema Mobeto.

No comments: