Friday, 28 November 2014

VIONGOZI WA AFRIKA WAASWA KUACHA KUNG'ANG'ANIA MADARAKA


Raisi wa Ufaransa Francois Hollande amewapa somo viongozi wa bara la Afrika,kwamba wanapaswa kujifunza kwa yale yaliyotokea nchini Burkinafaso na sio kung'ang'ania madarakani.

Kauli ya raisi Hollande imetoka katika mkutano wa nchi zinazozungumza kifaransa ,unaofanyika nchini Senegal,na kutolea mfano kwa kile kilichomkuta na kumuondoa madarakani Blaise Compaore na kutilia mkazo suala la katiba kuheshimiwa.



Akiipigia chapuo nchi yake ,Raisi Hollande amesema nchi yake iliepusha umwagikaji wa damu na kumsaidia Compaore kuokoa jahazi lililokuwa likielekea kuzama.

Maandamano makubwa yamepangwa kufanyika hivi leo nchini Togo wakati ambapo raisi Faure Gnassingbe anataka kuibadili katiba ya nchi hiyo ili aendelee kusalia madarakani.

Kufuatia kitendo hicho, raisi Hollande amesema kwamba muda wa Ufaransa kuingialia migogoro ya nchi zilizokuwa makoloni yake umekwisha kilichosalia ni kuona wale wote wanaozungumza kifaransa nchi zao zinafuata utawala wa kidemkrasia.

No comments: