Thursday, 18 December 2014

HAYA NDIO MAJANGA YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


HAYA MAJANGA! Wakati vuguvugu la uchaguzi wa serikali za mitaa likiwa bichi, baadhi ya sehemu zikiwa zinasubiri zoezi hilo kutokana na sababu tofauti, matukio mbalimbali, yakiwemo ya kusikitisha, yameripotiwa. 
 Wananchi wakiutoa mwili wa marehemu Bandoma Mabele (58) majini.

Huku washindi wa nafasi mbalimbali zilizokuwa zikigombewa wakisheherekea kwa namna ya aina yake, katika Kijiji cha Mwagika, Sengerema mkoani Mwanza, kulitokea msiba wa kusikitisha, baada ya mgombea wa nafasi ya Uenyekiti, aliyetambulika kwa jina la Bandoma Mabele (58) kufariki dunia kufuatia kuzama ndani ya maji ya ziwa Victoria. 


Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, Mabele alikuwa akisubiri kuwania nafasi hiyo kabla ya uchaguzi huo kuahirishwa, hali iliyomlazimu kuamua kwenda ziwani kuvua kwa ajili ya kitoweo akiwa ameongozana na vijana wawili waliotajwa kwa majina ya Paulini Ruchiri na Samweli Malulu. 

Baada ya kuingia ziwani, katika hali isiyotarajiwa, mtumbwi wao ulipata hitilafu na kupinduka na kuwafanya watu hao watatu kuanza kupigana kuokoa maisha yao, kitu ambacho kilimshinda mzee Mabele na hivyo kupoteza maisha.
Bw. Godfrey Ferdinand akiwa chakari. 

Wakati hali ikiwa hivyo mkoani Mwanza, jijini Dar es Salaam katika jimbo la Kawe, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Godfrey Ferdinand, alikutwa akiwa amelewa chakari, mfukoni mwake akiwa amechukuliwa vitu vyake vyote vya thamani. 

Habari kutoka eneo la tukio zinasema awali, jamaa huyo alikuwa ametoka kujiandikisha tayari kwa ajili ya uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita. Kana kwamba haitoshi, baada ya kutoka huko, alisikika akiwaambia marafiki zake kuwa waende sasa wakatumie, kwa vile alikuwa na fedha maana alipata mshahara kazini. 

Inadaiwa kuwa baada ya kuwa wamekaa mezani, watu aliokuwa nao walimzunguka na kumwekea vitu vilivyomzidishia kilevi na kujikuta akipoteza fahamu. 

Baada ya kupoteza fahamu ilidaiwa watu hao walichukua fedha zote alizokuwa nazo pamoja na vitu vingine vya thamani, wakimwacha na vitambulisho vyake tu! 

GEITA NAKO MAJANGA


Wakati hayo yakiendelea jijini Dar es Salaam, huko Geita nako hali ya hewa ilibadilika baada ya mgombea ujumbe wa mtaa wa Msalaba Road, huko Geita kwa tiketi ya Chadema, Beatha Mchimani Ngosha, ambaye alishinda, kukutwa ndani ya kisima akiwa ameshafariki. 

Ilidaiwa kuwa mshindi huyo alikuwa amekaa na wenzake wakisherehekea ushindi alipoaga kuwa anaenda kujisaidia, lakini hakurejea tena hadi mwili wake ulipokutwa kisimani asubuhi ya siku iliyofuata...

No comments: