Friday 19 December 2014

JOKATE NEXT LEVEL...ASAINI MKATABA WA BILIONI 8.5 NA KAMPUNI YA KICHINA KUMTENGENENZEA BIDHAA ZAKE ZA KIDOTI...


                                        

Mrembo Jokate Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya Kichina,  Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.

Makubaliano hayo yamesainiwa Dec 19 kwenye hotel ya Serena baina ya Jokate na Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited  (CEO), Deng Guoxun.
Akizungumza katika hafla hiyo,  Jokate alisema kuwa makubaliano hayo ni ya kudumu na kampuni hizo mbili zitazalisha na kuuza bidhaa za kidoti Tanzania nzima na nje ya mipaka yake.
Alifafanua kuwa kampuni ya China itawekeza Tanzania na kuwafaidisha watanzania kwa kutoa nafasi ya ajira. Alisema kuwa pia wanatarajia kujenga kiwanda ili kuinua uchumi wa nchi na maisha ya watanzania.
       

.
“Hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, kama unavyojua, wakati naanza kujishugulisha na masuala ya urembo, ubunifu na uanamitindo, sikutegemea kufikia hatua hii ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa, lakini sasa, ndoto zangu zimetimia na najivunia mafanikio haya,” alisema Jokate.
Alisema kuwa mbali ya kutoa mitindo tofauti ya kisasa ya nguo, kampuni yake pia itazalisha aina mbali mbali za viatu, nywele ikiwa pamoja na  mawigi,  weaving, Rasta na viatu vya wazi (sandals) ambazo kwa sasa zipo tayari kwenye soko la Tanzania.
“Mpango wangu ni kupanua soko la bidhaa zangu kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika Kusini na nchi nyingine za Afrika,” alisema.
Afisa Mtendaji  Guoxun alisema kuwa wamefurahi kukamilisha ubia na kampuni ya Kidoti na haya ni matunda ya ushirikiano wa kudumu baina ya serikali yao na Tanzania. “Tumefurahi sana kukamilisha makubaliano haya, tunatarajia kuongoza katika soko la hapa nchini na wenzetu (wachina) watafaidika pia, ” alisema Guoxun.  
Jokate akikabidhiwa mkataba wake......

Jokate akionyesha mkataba huo kwa waandishi na wageni waliohudhuria kwenye hafla hiyo...
   

No comments: