Thursday, 18 December 2014

Mh.RAIS AKIRI IDADI KUBWA YA WANACHUO UDOM KUWA NI MAKAHABA...

 

 Rais wa Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha UDOM Masatu Kyabwene amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Dodoma kujihusisha na biashara ya ukahaba kutokana na kukosa mikopo. Akizungumza na paparazi alisema“Kuna baadhi ya wanafunzi chuoni kwangu wana maisha magumu sana kutokana na kukosa mkopo,wakati mwingine wananifuata mimi na kunielezea shida zao ili niwasaidie,wengine ni yatima hawana baba wala mama wa kuwalipia ada,siyo siri maisha ya wanafunzi hawa ni magumu sana” Tatizo la kucheleweshwa kwa mikopo limekuwa sugu sana katika vyuo vikuu hapa tanzania ikiwemo chuo cha mzumbe morogoro ambapo wanafunzi wa mwaka wa pili hawajui hata lini watapata mkopo wao tangu wapate matokeo yao mitihani.
Nini maoni yako kuhusu jambo hili?

  ZIFUATAZO NI BAADHI YA PICHA ZA WANA VYUO WAKIWA KATIKA CLUB ZA USIKU WAKIFANYA YAO.........






No comments: