Tuesday, 16 December 2014

MAISHA HAYANA KANUNI...JOHARI AAMUA KUWA MUUZA NDIZI..MWENYEWE AFUNGUKA..


     
Muigizaji mkongwe wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amabae pia ni mkurugezi wa kampuni ya RJ ambayo inajihusisha na utengenezaji wa filamu hapa nchini.

 Hivi karibuni kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa INSTAGRAM aliweka picha hii hapa chini akionekana kichwani amejitwisha beseni lenye ndizi, yani kama mdada muuza ndizi anaetembea majumbani.
                      

Kwenye picha hii Johari aliandika kuwa hii ndio kazi yake mpya inayokuja japokuwa hakusema ni lini itakoka na hata jina la filamu hiyo hakulisema.

Johari aliandika maneno haya;
"Ujio mpya wa johari nikiwa mjasiriamali nauza ndizi dayana, we saka… mi nasaka pesa. heshima ya mtu pesa baby baby makelele".
Johari ni moja kati ya waigizaji wakike wenye uwezo na uzoefu mkubwa zaidi kwenye tasnia hii ya filamu na hivyo kujijengea heshma miongoni mwawaigizaji wakongwe na hata wapya huku mashabiki wake  wengi wakiendelea kumuunga mkono kwa kazi zake nzuri zenye ubora.
Mashabiki wengi walionyesha kuisubiri kwa hamu kaizi hii mpya, kwani ni kitambo sasa tangu Johari atoe mzigo mpya.

No comments: