Wednesday, 17 December 2014
TETESI:BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA...
Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa leo jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.
Waliotupwa nje kutokana na tuhumua za ufisadi ni pamoja na Anna Tibaijuka- aliyekuwa waziri wa ardhi nyumba na makazi, Sospeter Muhongo-aliyekuwa waziri wa nishati na madini huku Lazaro Nyalandu akihamishwa kutoka wizara ya mali asili na italii aliyokuwa akihudumu.
Walioondolewa kwenye wizara zao za awali na kuhamishwa ni pamoja na Lazaro Nyalandu ambaye anarudi mazingira. Saada Mkuya Salum kutoka fedha na kuhamishiwa ikulu pamoja na Gaudensia Kabaka.Hayo ni baadhi ya majina niliyopata.
Aidha rais Kikwete amewaondoa baadhi ya mawaziri katika baraza lake kutokana na uwajibikaji hafifu ambao ni Chiza Christophera-kilimo, Maghembe Jumanne-maji, Hawa Ghasia-tamisemi na Mathias Chikawe-utumishi Kikwete pia amewaingiza wengine wapya kwenye baraza la mawaziri ambao ni Serukamba Peter, Deo Filikunjombe na Kigwangala Khamisi.Hao bado haijafahamika ni wizara zipi walizoteuliwa.
Pia wapo waliopanda cheo kuwa mawaziri kamili ambao ni Simbachawene George, Mwanri, Godfrey Zambi, Mwigulu Nchemba, January Makamba na Greyson Lwenge. Hawa taarifa kamili ya wizara watakazohudumia tutawaletea.
Inasemekana kuwa Kikwete amepangua na kulipanga upya baraza lake kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyotarajiwa. Pia atamteua mkuu mpya wa sheria wa serikali ndani ya siku tatu zijazo kama nilivyodokezwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment