Monday 15 December 2014

HII NDIO KAULI YA KWANZA YA HAPPINESS WATIMANYWA BAADA YA KUTOFANIKIWA KUTWAA TAJI LA MISS WORLD

Baada ya Miss South Africa anajulikana kwa jina la  Rolene Strauss ambaye ndie mshindi wa taji la  Miss World 2014, Aliyekuwa akiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram amefunguka baada ya kushindwa kunyakua taji hilo na hichi ndicho alichokiandika


Nampongeza @rolenestrauss (South Africa) kwa kuibuka mshindi Miss World 2014.Watanzania wenzangu na marafiki kutoka mataifa mengine, tumepiga kura sana, mmeonyesha support kubwa kuliko matarajio ya wengi bahati mbaya kura hazikutosha. 
Natumia nafasi hii kuwashukuru wote mmoja mmoja kwa kuniunga mkono kwa kipindi chote ambacho nilikua hapa jijini #London na tokea niliposhinda mashindano ya #MissTanzania. Nisingefika hapa bila support yako. From deep inside my heart. I thank you.

Kuanzia aliyetumia muda na pesa yake kunipigia kura, aliyeandika na kutangaza habari yangu, designers mbalimbali, familia yangu, marafiki wote, wote, wote, I thank you. 
Nimejifunza vitu vingi sana kipindi chote hiki na kwakweli watanzania tumeonyesha umoja wa hali ya juu sana. Umoja wetu na udumu katika mambo yote ya kimaendeleo kwa taifa letu.

Mbarikiwe
#Happiness4MissWorld


No comments: