KATIKA hali ya kushangaza, wimbo wa msanii wa muziki wa dansi, Christian Bella ‘Obama’, umeonekana kuwa chanzo cha kutoweka kwa utulivu wa dakika kadhaa katika mazoezi ya Simba kwenye Gym ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Wimbo huo unaojulikana kwa jina la Nakuhitaji ambao unatamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga, ulipigwa na ndipo ukasababisha wachezaji kadhaa kulipuka kwa furaha kiasi cha kupoteza utulivu uliokuwepo eneo la tukio.
Championi Ijumaa lilikuwepo eneo hilo na kushuhudia wachezaji wakiwa makini muda mwingi kufuatilia mazoezi yaliyokuwa na hatua mbalimbali yakiongozwa na mwalimu anayewa
simamia katika mazoezi hayo, Hilary David, ghafla wimbo huo ulisababisha kelele na kila mmoja akionyesha utaalam wa kuuimba, licha ya kuwa siyo wote waliokuwa wakiuweza.
Baadhi ya wachezaji waliokuwa vinara wa kupiga shangwe baada ya wimbo huo ni; Ibrahim Ajib, Abdallah Seseme, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Abdulaziz Makame.
No comments:
Post a Comment