Friday, 19 December 2014
NDOA NDOANO: MCHEKI MAIMARTHA ALIVYOZEEKA
Mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’.
Mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’ ameibuka na kusema kuwa kitendo cha yeye kuingia kwenye maisha ya ndoa kimemsababisha sasa aonekane kama aliyezeeka kwani mambo mengi ya kisichana ameyaacha.
Akizungumzia maisha anayoishi Mai alisema, zamani alikuwa ikifika wikiendi anafikiria akajirushe wapi lakini sasa hivi imebaki historia kiasi cha baadhi ya mashosti zake kumtania kwa kumwambia, hana nyimbo na amezeeka.
“Kama ni suala la ndoa kunizeesha kweli imenizeesha, sasa hivi siyo yule Mai wa kila wikiendi kwenda kula bata, wapo mashosti ambao wananiponda kwa kubadilika kwangu lakini sijali, unajua kila jambo lina mwisho,” alisema Mai.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment