Monday, 15 December 2014

WEMA SEPETU ALICHUKIA NA KULITELEKEZA GARI ALILOZAWADIWA NA DIAMOND....



Ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond'.

LILE ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeanza kumchefua mrembo huyo kiasi cha kulisusa.Tukio hilo lilijidhihirisha wazi mbele ya paparazi wetu juzikati nyumbani kwa staa huyo, Kijitonyama jijini Dar, ambapo Wema alitamka hadharani kuwa kwa sasa analichukia kupita maelezo gari hilo alilozawadiwa na Diamond kwenye sherehe yake ya kuzaliwa. 
    

                                            Wema Sepetu akitafakari jambo.
 “Bwana acha nitumie hili gari lingine kwenda airport hilo Murano sitaki hata kulisikia, sijui najisikiaje hata nikiliona,”alisikika Wema.Paparazi wetu baada ya kusikia Wema akionesha wazi kuwa analichukia gari hilo, alimuuliza sababu inayomfanya alichukie ambapo alisema hajui ni kwa nini analichukia ingawa ni mali yake.


“Siku hizi sipendi kutumia hili Murano tena nalichukia kweli, inafikia kipindi nakosa raha nikiliona lakini ukiniuliza sababu ya kulichukia kiasi hicho hata sina sijui nimezoea sana kutumia BMW, ndiyo maana najikuta nalichukia gari hili,” alisema Wema.
     


                                                          Nasibu Abdul ‘Diamond'akipozi.
Kwenye bethidei yake iliyofanyika Septemba, mwaka huu, Wema alizawadiwa magari mawili. La kwanza lilikuwa ni BMW 545i (Sh. Milioni 56) ambalo liliibua utata juu ya mtu aliyemzawadia na la pili ni Nissan Murano (Sh. milioni 36) alilopewa na Diamond.

.

No comments: