KANISA LACHAGUA ASKOFU MWANAMKE KWA MARA YA KWANZA
Kanisa la Uingereza limemchagua askofu wa kwanza mwanamke.Mchungaji Libby Lane atakuwa askofu wa Stockport mnamo mwezi January ,na kumaliza ukiritimba wa wanaume kuwa maaskofu katika kanisa hilo.Amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo.Kanisa la Uingereza liliwachagua wanawake mara ya kwanza kama makuhani mnamo mwaka 1994.Wanawake tayari wameruhusiwa kuwa maaskofu katika maeneo mengine ya jamii ya kianglikana ,ikiwemo Marekani na kusini mwa Afrika.
CHANZO: BBC SSWAHILI
No comments:
Post a Comment