Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka amegoma kujiuzulu kwakuwa haoni sababu ya kufanya hivyo...
Akiendelea kuzungumza na waandishi muda huu anasema watu wanaona kujiuzulu ni 'fashion' ila yeye hayuko katika 'fashion' hiyo
Tibaijuka: Nikijiuzulu hata Rais atanishangaa maana katika yale mapendekezo ya Bunge hakuna sehemu iliyonitaka kujiuzulu.
Tibaijuka: Niliomba mchango wa Shule nikapewa na Rugemalira, sasa kujiuzulu nitakuwa sijaitendea haki jamii
Tibaijuka: Lengo la kuzungumza na Waandishi wa habari ni kuzungumza yale niliyokosa nafasi ya kujitetea wakati wa sakata la #TegetaEscrow
No comments:
Post a Comment