Thursday 18 December 2014

WEMA SEPETU AMCHANA KWEUPEEEE ZAMARADI MKETEMA WA CLOUDS ..


Mara baada ya mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha maswala ya filamu nchini cha TAKE ONE, Zamaradi Mtetema kuweka bandiko mtandaoni, akiwatata mashabiki na wapenzi wake, wataje mambo matano ambayo niyaukweli kuhusu yeye Zamaradi kwa jinsi wanavyomuona na atatoa zawadi kwa yule atakae patia.  Madam Wema Sepetu alikuwa ni mmoja kati ya watu waliojitokeza kwa kumwambia ukweli bila kumficha wala kusita na kutoa 5 facts za ukweli kabisa... 

Bandiko lilisema; 

"If someone managed kunitajia hata FACT 5 about me za ukweli kulingana na unavyoniona... nna zawadi yako kubwa and I AM SERIOUS.... Unahisi nikoje!!? only 5 facts then ntasema nani kapatia plus mentioning my other ones... okay legooooo " 

Baada ya watu kadhaa kujitokeza na kuanza kuzitaja, Muigizaji Wema Sepetu nae akaibuka na kuzitaja hizi; Unajipenda sana, Unampenda sana mwanao,Unapenda kupendeza,short tempered, na unapenda kupendwa. 

Hata hivyo Zamaradi aliibuka na kumwambia Wema kiutani kuwa asijisumbue kwani zawadi hawezi kupewa. 

Hivi nivijimambo tuu!!!.
      


No comments: