Saturday 20 December 2014

BAADA YA DIAMOND KUDAI MIMBA ALIZOMPA PENNY ZILIHABIKA KIUTATA! ZILIPENDWA HUYO AFUNGUKA KIIVI!


    
 
Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye.
Penny alitoa tamko hilo baada ya Diamond kunukuliwa na vyombo mbalimbalu vya habari na mitandao ya kijamii kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha. 
Akizungumza nasi hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi anapomuona mtoto anachanganyikiwa na kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi. 
“Kiukweli sasa ndiyo ule wakati wa kuzaa, natamani sana mtoto lakini sasa wa kuzaa naye yuko wapi? Hapo ndiyo tatizo maana siyo kuzaa na mtu ili mradi mtoto awe na baba,” alisema Penny.

No comments: