Thursday, 22 January 2015
ZIFAHAMU CLUB KUMI TAJIRI BARANI ULAYA,REAL MADRID YAFUNIKA
Real Madrid imeibuka kama klabu tajiri zaidi ulaya kulingana na orodha iliyotolewa na Deloitte Football Rich kwa miaka kumi mfululizo.
Manchester United imetoka nafasi ya nne hadi ya pili katika orodha hio, kulingana na mapato ya msimu wa 2013 -2014
Bayern Munich, Barcelona na Paris St -Germain walifuatana kwa orodha hiyo kutoka nambari tatu.
Klabu za Uingereza, Machester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool wanafuatana kutoka nambari sita hadi tisa, wote wakionyesha dalili nzuri za kuongeza mapato .
Klabu za Uingereza, Machester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool wanafuatana kutoka nambari sita hadi tisa, wote wakionyesha dalili nzuri za kuongeza mapato
Totenham wanashikilia nambari 13, huku Newcastle United wakikaribishwa kwa orodha ya ishirini bora katika nafasi ya 19 na ishirini.
Kwa pamoja, mapato ya vilabu 20 bora yaliongezeka kwa asilimia 14 kufikisha pauni bilioni 6.2, ripoti hiyo ilisema.
Kulingana na ripoti hiyo,inaangazia mapato pekee bila madeni.
Real Madrid, ambayo ilishinda kombe la klabu bingwa Ulaya mwaka jana, kwa kuwacharaza majirani wao Atletico Madrid 4 - 1, waliweza kuona mapato yao yakiongezeka kwa pauni milioni 49.5 kwa kiwango wastani cha fedha kwa mwaka ulioisha Juni 30, 2014.Klabu hio iliweza kupata ongezeko la mapato ya pauni milioni 30.6 kutokana na asimilia 8 za matangazo na asilimia 9% kutokana na biashara
" Galatasary ilikuwa kilabu ya pekee kuorodheshwa katika 20 bora licha ya kusakata dimba nje ya ligi tano bora huko ulaya.
" Klabu ya Italia Napoli ilijibwaga katika orodha ya ishirini bora baada ya mapato yao kuongezeka na zaidi ya asilimia 50
" Klabu ya Atletico Madrid iltoka nafasi ya 20 hadi 15 baada ya kufika katika fainali ya klabu bingwa ulaya
KUMI BORA
1. Real Madrid: Pauni Milioni 549.5m)
2. Man Utd: Pauni Milioni 518m
3. Bayern Munich: Pauni Milioni 487.5m
4. Barcelona: Pauni Milioni 484.6m
5. Paris Saint Germain; Pauni Milioni 474.2m
6. Manchester City: Pauni Milioni 414.4m
7. Chelsea: Pauni Milioni 387.9m
8. Arsenal: Pauni Milioni 359.3m
9. Liverpool: Pauni Milioni 305.9m
10. Juventus: Pauni Milioni 279.4m
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment