Thursday, 22 January 2015

JOKATE AMFUNIKA LULU,MWENYEWE AFURAHIA

 Mwanamitindo na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo 

MWANAMITINDO na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo amekuwa tishio kwa msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa urembo na muonekano katika picha zinazoonekana mitandaoni nchini. 


Moja kati ya mitandao mikubwa ya hapa nchini uitwao Kandili Yetu uliendesha zoezi la kuweka picha zao kali zinazowaonesha wote wawili wakiwa na muonekano na picha kali huku wakiuliza nani zaidi ya mwenzake.Jokate ameibuka mshindi kwa kupigiwa kura nyingi huku watu wakimsifia kuwa ni wa kimataifa zaidi ambapo Lulu alionekana kupigiwa kura na watu wachache. 
     

Msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’. Amani liliongea na Jokate ambaye aliwashukuru Watanzania kwa kumpenda na kumpa nafasi lakini aliwasihi kwa kuwaambia kuwa yeye aonavyo wote ni warembo.“Mimi naona sisi wote ni warembo, nawashukuru Watanzania walionichagua na kuniona nafaa,” alisema Jokate
Lulu alipotafutwa, hakupatikana. 
Chanzo;Gazeti la Amani

No comments: