Sunday, 18 January 2015

LULU: SICHANGANYI MADAWA KAMA WENGINE,NITABAKI KUWA MUIGIZA


MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema katika maisha yake ya sanaa hataweza kuchanganya madawa kufanya kazi nyingine mbali na kuigiza kama ambavyo wasanii wengine wanafanya. 


Akipiga stori na mwandishi wetu, Lulu alisema, amegundua kuwa kila kitu kinatakiwa kifanywe kama kazi na yeye atakuwa akifanya kazi yake ya kuigiza tu na si vinginevyo.
“Napenda kuwa msanii na ninaamini mimi ni msanii, niweke wazi kwamba mimi katika maisha yangu sitarajii kuja kuwa dairekta au script writer wala kuja kufanya kazi nyingine yoyote zaidi ya kuigiza.
“Asilimia kubwa ya wasanii hapa kwetu hatuwazi mbali, chochote tunachofanya tunaona ni sawa tu hatupo kibiashara kwa sababu bado ni masikini ndiyo maana wengine wanaigiza ili waonekane, tubadilike,” alisema Lulu.

No comments: