Sunday, 21 December 2014

HATA UWE PEDESHEEE KIASI GANI,KAMA HAUKO TAYARI KWA "MAMBO FLANI" HUWEZI KULA MZIGO KWA SHILOLE (SHISHI BABY)

Mwigizaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Zuwena Mohamed, maarufu kama shilole amedai kuwa anaweza kufanya ujinga wowote humu duniani lakini linapokuja suala la mapenzi hapo yupo makini sana na kamwe hawezi kufanya ujinga wa kujisahau au kukurupuka tu kwa kumuangalia MTU alivyo kwa uzuri au pesa zake... 
Aliweka wazi kuwa kamwe hawezi kwenda kwenye mtanange bila kutumia zana ama pekupeku kama watoto wa mjini wanavyosema kwani anaogopa sana gonjwa hili lisilotibika la UKIMWI ambalo limewamaliza mastaa kadhaa nchini na bado linaendelea kuwatafuna wengi waliosalia.

Akiongea alisema kuwa hata mtu awe vipi, au awe wa dini gani au awe na pesa kiasi gani kamwe hawezi kumkubalia kufanya naye kitendo hicho kilichokatazwa kabla ya ndoa bila kutumia kinga na alizilaani kauli zinasema eti ukitumia kinga ladha ya mapenzi inapungua kuwa si za kweli na za kijinga.

“Unajua nini mwandishi, najipenda na nayapenda maisha yangu, mimi ni mrembo, nisipojilinda nani atanilinda?” Aliongeza Shilole Hata niwe nimelewa kiasi gani huwa nipo makini sana maana najua vijana wengi wa mjini wananimendea sana,hivyo kama mtu hataki kuvaa Condom hawezi pata mautam hapa” Alizidi kusisitiza mrembo huyo.




No comments: