Kocha mpya wa Yanga Hans Pluijm leo amefanya mkutano wa kwanza na waandishi wa habari tangu apewe mikoba ya kuifundisha tena timu hiyo yenye maskani mitaa ya Kariakoo jijini Dar Es Salaam.
Mkutano huo umefanyika Jangwani, kifupi alichosema ni kwamba amefurahi kurudi Yanga paia amesisitiza kuendeleza utamaduni wake wa kufundisha soka la kuvutia ikiwa ni pamoja na kushambulia, mambo ambayo yatawafanya wanayanga kuwa na furaha,amesema amewaambia wachezaji wake kwamba hakuna mafanikio ya mtu mmoja,iwapo watajituma na kuwapa ushirikiano benchi la ufundi pamoja na viongozi basi mafanikio mengi yatakuja.
Van Pruijm anasema anajua kazi kubwa iliyopo mbele yake hasa mchezo ujao dhidi ya azam na kesho wanaingia kambini kujiwinda na mchezo huo.
No comments:
Post a Comment