Saturday, 27 December 2014

WAKAMATWA KWA KUIBA SANAMU YA BIKIRA MARIA...



Vijana watatu Songea wametakiwa kwenda na wazazi wao kutubu dhambi za kutaka kuiba sanamu la Bikira Maria katika Kanisa Katoliki la Kigango cha Samora. 


Katekista wa Kigango hicho Keneth Mhagama walisema vijana hao walifanya jaribio hilo usiku wa manane baada ya ibada ya mkesha ambapo walinzi walifanikiwa kuwadhibiti kabla hawajafanikiwa na wakawekwa mbaroni.

Vijana hao ni Ahmed, Mohammed na Leonard ambapo Padri wa Kanisa hilo Cristom Kapinga amesema vijana hao wanatakiwa kutubu la sivyo watawaacha kwenye mikono ya sheria washughulikiwe.

No comments: