Wednesday, 24 December 2014
KAOLE SANAA GROUP LAFUFUKA TENA,LABATIZWA JINA JIPYAAAAAA....
Kundi kongwe la sanaa ya uigizaji na ngoma lililotoa vipaji vingi vya uigizaji hapa nchini, Kundi la Sanaa la Kaole “Kaole Sanaa Group” limerudi ila sasa kwa jina lingine..habari kamili ametueleza hapa, Halima Yahya “DAVINA”moja kati ya waliokuwa kaole na sasa wameasisi hii kaone, anasema;
"Wapenzi wetu wa tamthilia na filamu za kibongo...mimi km mimi nimekua nikipokea maoni ya watu wengi hapa na hata mikoani kwamba wamemiss tamthilia zetu za zamani zilizokua zimejaa maadili na mafundisho nami kwa kushirikiana na wenzangu kadhaa tuliokua ktk kundi la maigizo la KAOLESANAAGROUP tumeamua kulirudisha kundi ila kwa sasa litaitwa KAONE na tutakuemo wasanii wengi wa zamani kidogo akiwepo Nyamayao, kibakuri, Muhogo Mchungu, bi Star, Thea,Coletha,Ndumbagwe na wasanii kibao uwajuao."
Pia akaeleza siku ya uzinduzi rasmi wa kundi hilo;
“Tutalizindua rasmi kundi letu cku ya tar 26 meezi huu wa 12 pale Darlive Mbagala mtapata kuona mengi tuliyowaandalia pia na tamthilia yetu mpya iitwayo KIPUSA itakayoanza kuruka hewani tarehe 5 mwezi wa kwanza katika kituo cha televisheni cha Tv1.
Karibuni sana sana na tunawaahidi vitu adimu mlivyovikosa muda mrefu....tunawapenda san bila nyinyi hakuna sisi"....Davina alimaliza.
Pichani ni baadhi ya wasanii wanaounda kundi hilo, wakiwemo, Davina, Nyamayao nawengineo.Ngoja tusubiri tuone moto wao...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment