Saturday, 27 December 2014
MMTALAKA WA MBUNGE AWASHANGAA WANAOMWITA MBURULA...
Mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya mjini Mh.Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’, Faiza Ally.
Mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya mjini Mh.Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’, Faiza Ally amefunguka kuwa, watu wasidhani kuwa yeye ni mbulula kwa uamuzi wake wa kuvaa pempasi ukumbini bali aliamua tu.
Akipiga stori nasi juzikati, Faiza alisema ameshangaa kuona watu wanaona ni ishu kwake kuvaa vazi hilo na alifanya vile makusudi kuonesha kuwa ni siku yake ya kuzaliwa na hivyo siku hiyo alikuwa kama mtoto.
Faiza Ally. “Jamani mimi siyo Mbulula wa kuvaa vile kama baadhi walivyosema, mimi nina uamuzi wa kuvaa chochote ambacho najiskia.
“Kuvaa vile ilikuwa ni katika kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa, mbona marafiki zangu hawakuona kuwa ni jambo baya?” alisema Faiza ambaye hivi karibuni alitinga kwenye Ukumbi wa Sea Cliff uliopo Masaki jijini Dar akiwa amevaa pempasi na kitop, jambo lililozua gumzo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment