Monday, 22 December 2014

Mh ANNA TIBAIJUKA KUMGOMEA RAIS KIKWETE???????


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete amemaliza hutuba yake na Wazee wa Jiji la Dar es salaam na Kumalizia kwa Kumuwajibisha waziri wa Ardhi na Makazi, Anna Tibaijuka kwa kutengua wadhifa wake wa UWAZIRI.mh rais alisema "Waziri Tibaijuka alifanya makosa kimaadili; tumemwomba AnnaTibaijuka apumzike tumteue mwingine!"
Pia Mh Rais amesema kuwa "Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo huyu nimemuweka kwanza kiporo maana bado uchunguzi unafanyika"...
Siku za hivi karibuni waziri Tibaijuka aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuwaeleza bila kusita kuwa HAWEZI KUJIUZURU KWANI SIO FASHENI KWA KUWA YEYE HANA KOSA.....Leo mkutano na wazee wa mkoa wa Dar es salaam,Rais Jakaya KikweteKikwete ametaja kosa alilofanya mh Anna Tibaijuka kuwa ni KUKIUKA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA...Je Mh Anna Tibaijuka atambishia mh Rais kuwa hakutenda kosa hiloooooo????????

No comments: