Saturday, 27 December 2014
TAARIFA KAMILI YA BOMU LILILOLIPUKA HUKO RUVUMA NA KUMUUA MLIPUAJI
Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akitoa maelezo kwa DCP Diwani Athumani ambaye aliwasili mkoani humo jana kwaajiri ya bomu la kutengenezwa kienyeji ambalo askari wa doria walinusurika kurushiwa na kumlipukia mlipuaji wa bomu hilo ambaye
alifariki papo hapo.
Askari WP Mariam mwenye namba 8616 akiwa amelazwa wodi ya majeruhi hospitali ya Mkoa baada ya kujeruhiwa mkono wa kushoto kwenye bega baada ya vipande vya bomu kumfikia akiwa na askari wenzake kwenye doria siku ya sikukuu ya krisimas.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiuangalia mwili wa mtuhumiwa wa ulipuaji wa bomu ambaye alitaka kuwarushua askari wa doria wakati wa sikukuu ya krismas kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. (PICHA NA AMON MTEGA ,SONGEA.
.....................................................
NA AMON MTEGA,SONGEA
JESHI la Poilisi mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na timu ya makachelo toka makao makuu ya jeshi hilo wanawasakaka watu watatu ambao wanasadikiwa kujihusisha na ulipuaji wa mabomu huku mwenzao mmoja akiwa amefia katika eneo la tukio baada ya kutaka kufanya jaribio la
kuwatupia bomu bomu askari waliyokuwepo doria katika sikukuu ya Krisimas ambalo lilimshinda na kumlipukia mwenyewe na kusababisha kupoteza maisha papo hapo huku utumbo ukiwa umemwagika nje na mkono wake wa kushoto ukiwa umekatika kabisa na vipande vyake hajijulikani vilipo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano wa jeshi la polisi Mkoa wa Ruvuma Naibu Kamishna wa jeshi la Polisi, kaimu mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jina nchini (DCP) Diwani Athumani alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 1.30
usiku huko katika mtaa wa Kotazi uliopo kata ya Majengo manispaa ya Songea ,timu ya askari wakiwa doria kulitokea mlipuko wa kitu kinachozaniwa kuwa ni bomu ambalo limetengenezwa kienyeji na kusababisha kuwajeruhi askari wawili .
DCP Athumani aliwataja askari waliojeruhiwa kuwa ni PC Mselem mwenye namba G 7903 ambaye alijeruhiwa mkono wake wa kushoto na alitibiwa na kuruhusiwa na mwingine PC Mariam mwenye namba WP. 8616 ambaye amejeruhiwa kwenye bega la mkono wa kushoto na amelazwa katika hospitali ya Mkoa Songea(HOMSO)akiendelea kupata matibabu.
Alisema kuwa timu ya makachelo toka makao makuu wakishirikiana na makachero wa Mkoa wa Ruvuma wamejipanga vizuri kuhakikisha watuhumiwa watatu waliohusika na tukio hilo pamoja na kufuatilia mtandao wake wa hualifu wanakamatwa mara moja kwani vitendo vya ulipuaji wa mabomu umekithiri nchini ikiwemo Mkoa wa Ruvuma kwani hadi sasa ni tukio la
tatu kwa mwaka huu.
DCP Athumani alieleza zaidi kuwa wahalifu hao watakamatwa kirahisi kutokana na tukio walilolifanya baada ya mwenzao kulipukiwa na bomu hilo na kusababisha kifo chake walijaribu kutorosha mwili wa mwenzao ili kupoteza ushahidi lakini ilishindikana baada ya askari polisi
doria wengine kuwahi eneo la tukio na wahalifu hao waliacha mwili wa
mwenzao na kutokomea kusikojulikana.“Wahalifu hao waliuvuta mwili wa mwenzao kutoka katika eneo la tukio kwa umbali wa mita zisizopungua 80 na 90 kwa lengo la kutaka kupoteza
usahidi lakini waliwahiwa na askari wengine wa doria na kuuacha mwili na kutokomea kusikojulikana” alisema DCP Athumani.
Hata hivyo amewaomba wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini,wanasiasa,wazee, makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na waandishi wa habari kuwa kitu kimoja katika kuwafichuwa waharifu hao ili matukio hayo yasiweze kujirudia tena hususani Mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu aliyetembelea
eneo la tukio na kuzungumza na waandishi wa habari kwa masikitiko
makubwa alisema kuwa waharifu hao wanaishi kwenye jamii inayotuzunguka
hivyo ni vyema kila mmoja akaliona jambo hili kwa umuhimu wake wa
pekee kulipa uzito na kuwafichuwa wahalifu ili Mkoa uendelee kuwa na
amani kwani linaleta taharuki kwa jamii jambo ambalo linarudisha nyuma
shughuli za maendeleo.
Naye Mganga Mkuu mfawidhi Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Dkt. Benedkto
Ngaiza amethibitisha kupokea mwili mmoja wa mtu ambaye amekufa ukiwa
utumbo umetoka nje na majeruhi wawili ambao ni askari na kwamba
askari mmoja alitibiwa jana na kuruhusiwa huku mmoja akiwa amelazwa
wodi ya majeruhi namba mbili akiendelea kupatiwa matibabu na hali
yake inaendelea vizuri.
CRT: DEMASHO.COM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment