Sunday, 21 December 2014

UTAFITI MZITO NA UCHAMBUZI WA STATUS ZA WHATSAPP HUU HAPA....

   
Habari za weekend wadau wangu....Najua wengi wenu mmejipumzisha na pia kuna  mnaoendelea na kupiga mishemishe...Mungu awabariki..
Leo katika pita pita zangu nikakutana na utafiti huu ambao naamini sio wa kisayansi lakini ni muhimu kukushirikisha....Utafiti huu unahusu Status mbalimbali zinazopatikana kwenye profiles mbalimbali kwenye mtandao wa WHATSAPP...Bila kupoteza muda naomba tuungane kuzifuatilia status hizo na uchambuzi wake yakinifu:

"I luv u dady, can't wait to 've ur f" (Unakuta ni uzushi tu, hakuna chochote, hajaolewa wala nini, kama sio ufuska ni nn?) 

"Oh baby, I can't forget that f u gave me last night" (Sijui alikutana na mtu tu akamnyapua, yeye tayari keshaanza kumpublish kama baby)
"We are the real lovers, no one can separate us" (Unakuta ndoa inatemblea drip, ina migogoro balaa)
"luv luv luv u my husband, u know ur a gentleman" (Mkianza kuchat anamdis jamaa)


"This is my beloved son, he was born when his father was going to Europe, so two in one!" (Europe tandika! Hajui hata Airport iliko!)

"Kill them with succes n burry them with Smile" (Unakuta mambo yamemgomea, hasa vitoto vya shule, may be hata amedisco, mafanikio yatakuwa yake!)

"I'm single but this does not mean I'm available" (Hapa amechakazwa, hadi hajijui status yake!)

etc, etc, etc.,

Bado wale wanaojipa matumaini na kujifanya mara wanampenda Mungu sana, sijui Yesu na wakati hata hawamjui!

UGUNDUZI WA MTAFITI...

Baada ya kufanya research kuhusu hawa watu hasa wa WhatsApp ndipo nilipogundua yafuatayo:

1. Wanaoandika message kuonyesha wanawapenda wenzi wao, wala hawawapendi - ukiwapa tu nafasi ya kuchat wanaanza kuandika maneno ya usaliti kuhusu wapenzi wao

2. Wanaoandika msgs kujifanya wamewamiss wenzi wao - hawana hata wapenzi wa kusingizia, wanajifariji baada ya kukataliwa, wewe waruhusu tu kidogo waongelee habari ya mapenzi, mbona majanga!

3. Wanaoandika msgs kali kali kuhusu mapenzi e.g. "leave me alone", "Kwani mapenzi/mwanaume kitu gani" - wametendwa baada ya kuwavamia wanaume kichwakichwa

4. Wengine wanaandika msgs kama vile "Sexy me", "love myself", - hawa wanatafuta attention ya wanaume na kujaribu kujipandishia self esteem.

5. Bado wale wanaoweka picha za magari, majumba na kuandika "Hapa ndio kwa hubby", sijui "I'm tired driving this BMW thing, need to change a car!", - hawa wanataka kujionyesha kuwa mambo yao safi hata wasipoolewa maisha yatasonga kwa nguvu ya wallet.
UNA MAONI GANI JUU YA UTAFITI NA UCHAMBUZI HUU????...


No comments: