Thursday, 18 December 2014
WEMA SEPETU AMCHANA KWEUPEEEE ZAMARADI MKETEMA WA CLOUDS ..
Mara baada ya mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha maswala ya filamu nchini cha TAKE ONE, Zamaradi Mtetema kuweka bandiko mtandaoni, akiwatata mashabiki na wapenzi wake, wataje mambo matano ambayo niyaukweli kuhusu yeye Zamaradi kwa jinsi wanavyomuona na atatoa zawadi kwa yule atakae patia. Madam Wema Sepetu alikuwa ni mmoja kati ya watu waliojitokeza kwa kumwambia ukweli bila kumficha wala kusita na kutoa 5 facts za ukweli kabisa...
HAYA NDIO MAJANGA YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
HAYA MAJANGA! Wakati vuguvugu la uchaguzi wa serikali za mitaa likiwa bichi, baadhi ya sehemu zikiwa zinasubiri zoezi hilo kutokana na sababu tofauti, matukio mbalimbali, yakiwemo ya kusikitisha, yameripotiwa.
Wananchi wakiutoa mwili wa marehemu Bandoma Mabele (58) majini.
Huku washindi wa nafasi mbalimbali zilizokuwa zikigombewa wakisheherekea kwa namna ya aina yake, katika Kijiji cha Mwagika, Sengerema mkoani Mwanza, kulitokea msiba wa kusikitisha, baada ya mgombea wa nafasi ya Uenyekiti, aliyetambulika kwa jina la Bandoma Mabele (58) kufariki dunia kufuatia kuzama ndani ya maji ya ziwa Victoria.
BI.CHEKA ANAHITAJI MSAADA WA HARAKA
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Bi Cheka hivi sasa ni mgonjwa. Anahitaji matibabu na huduma muhimu kutokana na umri wake mkubwa
(ana miaka 55).
Hali yake kimaisha ni mbaya, kwani anaishi katika kibanda cha udongo, yeye na wajukuu zake. Global Publishers inaendesha harambee hii ili aweze angalau kujenga kibanda cha bati na kupata matibabu.
Mchangie chochote ulichonacho, iwe 500, 1000, 5000 au zaidi kupitia namba 0654 880 707. Kitakachopatikana mtatangaziwa. Kutoa ni Moyo!
Wednesday, 17 December 2014
TETESI:BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA...
Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa leo jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.
Waliotupwa nje kutokana na tuhumua za ufisadi ni pamoja na Anna Tibaijuka- aliyekuwa waziri wa ardhi nyumba na makazi, Sospeter Muhongo-aliyekuwa waziri wa nishati na madini huku Lazaro Nyalandu akihamishwa kutoka wizara ya mali asili na italii aliyokuwa akihudumu.
Walioondolewa kwenye wizara zao za awali na kuhamishwa ni pamoja na Lazaro Nyalandu ambaye anarudi mazingira. Saada Mkuya Salum kutoka fedha na kuhamishiwa ikulu pamoja na Gaudensia Kabaka.Hayo ni baadhi ya majina niliyopata.
UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA: AFUKUZWA BAADA YA KUMSHINDA BABA MWENYE NYUMBA
VITUKO vinazidi kuripotiwa katika chaguzi za serikali za mitaa zinazoendelea nchini na mjini Morogoro, mgombea kutoka muungano wa Ukawa, Sharrif Abdul Mnola (Chadema) ametimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa anaishi baada ya kumshinda mpinzani wake, Makalla Salum Hassan (CCM) ambaye ni mmiliki wa mjengo huo uliopo mtaa wa Ngoma ‘A’ kata ya Mji Mpya.
Sharrif ambaye ni dalali wa magari alishinda baada ya kupata kura 79 huku Makalla akipata 72.
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AJIUZURU..SOMA SABABU ALIYOTOA..
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia jana,Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
Tuesday, 16 December 2014
MAISHA HAYANA KANUNI...JOHARI AAMUA KUWA MUUZA NDIZI..MWENYEWE AFUNGUKA..
Muigizaji mkongwe wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amabae pia ni mkurugezi wa kampuni ya RJ ambayo inajihusisha na utengenezaji wa filamu hapa nchini.
MTUHUMIWA WA WIZI WA PIKIPIKI ANUSURIKA KUUAWA MAGOMENI LEO HII....
KIJANA ambaye jina lake haikufahamika mara moja, amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kwa tuhuma za wizi wa pikipiki jijini Dar.Tukio hilo la kusisimua limetokea asubuhi ya leo Magomeni-Mwembechai, ambapo lilisababisha foleni ndefu ya magari wakati kijana huyo akiadhibiwa na wananchi.
Subscribe to:
Posts (Atom)