Thursday, 4 December 2014

BAADA YA DIAMOND KUTWAA TUZO 3 CHANNEL O PRODUCER WAKE AANZA KUTOA MALALAMIKO


Producer wa hits mbili za Diamond Platnumz ‘Number One’ na ‘Ntampata Wapi’ alionekana kufurahia mafanikio ya Diamond kwenye tuzo za Channel O, lakini kitu kimoja hakijakaa sawa moyoni mwake hivyo ameamua kutoa lake la rohoni...

MGOGORO WA MPAKA KATI YA TANZANIA NA MALAWI..HALI BADO NI TETE



Kile kilichoonekana kuanza kama mzaha kati ya Tanzania na Malawi kuhusu umiliki wa Ziwa Nyasa, sasa kimeanza kuchukua sura mpya kwa kila nchi kuendelea kutekeleza kitu inachokiamini kuwa ni sahihi.

KOREA KASKAZINI YAISHUTUMU MAREKANI KWA KUTENGENENZA NA KUSAMBAZA VIRUSI VYA EBOLA BARANI AFRIKA


Koreas Kaskazini imeishutumu Marekani kwa kusambaza makusudi virusi vya ugonjwa wa Ebola na kwamba inatengeneza silaha hiyo ya kibailojia ili kuwa taifa lenye nguvu zaidi duniani.

CHELSEA NOMA....YAICHAPA TOTTENHAM 3-0.....

 

LHRC YASIKITISHWA NA KAULI YA PINDA KUWA HANA UHAKIKA FEDHA ZA ESCROW NI ZA NANI..


Kituo cha sheria na haki za binadamu kimesema kimesikitishwa na kauli aliyoitoa waziri mkuu Mh Mizengo Pinda bungeni wakati akiahirisha bunge kuwa hakuna uhakika kwamba fedha zilizokuwa katika akaunt ya Escrow kama ni za serikali ama la jambo ambalo amesema kwa kufanya hivyo ni kutaka kuwalinda waliohuska katika wizi huo.
 

UKAWA WAANZA KUSALITIANA ARUSHA


VYAMA vinne vya upinzani vilivyoungana na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vimeshindwa kuachiana nafasi za uongozi mkoani Arusha, katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14.

Mh.ZITTO KABWE APATA MCHUMBA


MBUNGE Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amemtambulisha mchumba wake mpya anayetarajia kufunga nae pingu za maisha hivi karibuni. 

188 WAHUKUMIWA KIFO NCHINI MISRI


Mahakama moja ya Misri imewahukumu kifo wafuasi 188 wa harakati ya Ikhwanul Muslimin kwa madai ya kuhusika kwenye shambulio lililotokea mwaka 2013 katika kituo cha polisi mjini Cairo. Hukumu hiyo ilitangazwa hapo jana ambapo watu hao wanadaiwa kushambulia na kuua askari kadhaa wa usalama.  Wakati huo huo maelfu ya wananchi wa Misri wameandamana nchini humo kupinga uamuzi wa mahakama wa kumfutia mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili dikteta wa zamani wa nchi nchi hiyo Hosni Mubarak.

Waandamanaji hao huku wakitoa nara za kupinga serikali na kulaani utawala wa kijeshi wa Misri, wamesema kuwa hawatosalimu amri hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa. Polisi ya Misri imefunga barabara zote zinazoelekea katika Meidani maarufu ya mjini Cairo ambako hukusanyika waandamanaji, baada ya kuanza wimbi jipya la malalamiko ya wananchi ya kupinga kufutiwa mashtaka Hosni Mubarak.