Saturday 17 January 2015

WANAOPENDA KUPIGA PICHA ZA SELFIE KUMBE WANA TABIA HII YA KIPEKEE....


Kuna utafiti uliofanywa na Ohio State University Marekani, unahusu masuala ya athari zinazoweza kusababishwa na watu kupendelea kupiga Selfie na kupost kwenye mitandao kama Istagram. 

Jumla ya watu waliofanyiwa utafiti huo walikuwa 800, umri wao ulikuwa kati ya miaka 18 na 40. 

Matokeo yanaonyesha kuwa watu wanaopenda kujipiga Selfie wakiwa peke yao wanakuwa na tabia ya ubinafsi na hawapendi kujichanganya na watu wengine. 

Tabia hiyo inaonenaka ‘imekomaa’ zaidi kwa wale wanaopenda kuedit Selfie zao kabla hawajapost kwenye mitandao. 

Hayo ni matokeo yao, wewe unasemaje hapo mtu wangu, eti ni kweli?

No comments: