Wednesday, 14 January 2015

MBIO ZA URAIS,BODI YA WAKURUGENZI NHC VILISABABISHA PROF TIBAIJUKA AFUKUZWE KAZI,SAKATA LA ESCROW LATUMIKA KAMA KIVULI.

Ndugu zangu,wananchi wenzangu na watanzania wenzangu na wapenzi wa blogu hii,inafahamika kuwa aliyekuwa Waziri wa Kazi,Nyumba na Mandeleo ya Makazi Prof Tibaijuka alifukuzwa kazi  kutokana na ukosefu wa Maadili kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete alivyodai, 


Rais Kikwete alitangaza kumfukuza kazi Mbunge huyo wa Muleba Kusini (CCM)katika Mkutano wake wa Wazee wanaokaa mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika Jijini Dar Es Salaam,ambapo Rais Kikwete alisema Waziri huyo alipokea zaidi ya Bilioni 1.6 kutoka kwa Mbia wa Kampuni ya IPTL,Bwana James Rugimalira ambapo ni Kinyume na Maadili ya utumishi wa Umma.

Licha ya Profesa Tibaijuka kujinadi katika Mkutano wake na Wandishi wa Habari aliouitisha na Kujinadi kwamba hawezi kujiuzulu kwenye Nafasi ya Uwaziri kwa Madai hakuhusika kwenye wizi wa zaidi ya Bilioni 306 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa BOT.

Taarifa za Kuaminika ambazo Mtandao huu umezipata zinasema Shinikizo la kufukuzwa Prof.Tibaijuka limepewa nguvu na baadhi wa makada kutoka ndani ya chama cha Mapinduzi akiwemo spika wa bunge Anna makinda ambao wanamwona tishio katika harakati zake za kutaka kumrithi Rais anayemaliza mda wake Jakaya kikwete mwakani 2015.

Kwa Mujibu wa Chanzo chetu cha kuaminika kinasema Profesa Tibaijuka alikutana na Rais Kikwete Ikulu siku chache kabla ya ule mkutano wa Rais na wazee waishio Dar es salaam kufanyika ambapo katika mazungumzo yake Mtoa taarifa huyo anasema Prof Tibaijuka alimueleza Rais Jakaya Kikwete Hatua kwa hatua jinsi Fedha zilivyotolewa na Rugimalira hadi kupelekwa kwenye  Akaunti ya shule..... 

Aidha,katika Kikao hicho Rais Kikwete alikubaliana na Prof Tibaijuka na akamtaka akaitishe mkutano na Waandishi wa Habari ili kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.
Na ndivyo Prof Tibaijuka akaitisha  mkutano wake na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Hyatt Regency (KILIMANJARO)
    Akilielezea hilo Ofisa mmoja wa Ikulu alinukuliwa na chanzo kimoja cha Habari alisema baada ya kukutana na waandishi wa Habari, aliitwa tena Ikulu,safari hii alikutana na Makamu wa Rais Dk,Mohamed Gharib Bilali na Waziri Mkuu mizengo Pinda.

“Walipofika hapa Ikulu,Prof Tibaijuka alikutana  na Rais Kikwete Dk Bilali na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakamwambia kuwa Jinsi hali ya Hewa ilivyochafuka ni vema akawapisha kwa kujiuzulu yeye alikataa”
“Akasema hawezi kurudi tena kwa wananchi kuwambia anajiuzulu kufanya hivyo ni kugeuka jiwe ,kama wao wanamwona afai,basi wamfukuze kazi  lakini siyo kujiuzulu”aliileza Ofisa huyo Mwandamizi wa Ikulu ambaye akutaka Jina lake litajwe mtandaoni.

Mbali na hivyo Taarifa Zengine ambazo Mtandao huu zilipata pamoja na Nyaraka mbalimbali zinamwonyesha Profesa Tibaijuka akipigania Uwaziri Tangu Sakata hili lilivyokuwa Bungeni,lakini viongozi wa Bunge wakiongozwa na Spika Anne Mkinda walimyima haki hiyo ndio maana Rais Kikwete alipogundua kwamba Bunge lilimyima haki ya Kujitetea ndipo akamtaka akajitete kwa wananchi.

Akiandika kwa Spika Makinda tarehe 20 Novemba 2014 Prof Tibaijuka alisema  “Pamoja na kuomba kuchangia  kupitia Mhe Jestina Muhagama –Katibu wa Bunge wabunge wa CCM-hadi sasa hakuna uhakika kama nitapewa nafasi hiyo kabla hoja kufungwa’
       
 Barua hiyo kwenda kwa Spika Makinda ilikuwa na kichwa cha Habari hivi  “Muda wa Kujitetea mbele ya Bunge kufuatana na kutajwa kwa jina langu katika Taarifa ya PAC –Issue ya Escrow



Katika kile kinaoneka ni kwamba Spika Makinda alikuwa anataka kumsulubu Msomi huyo alimjibu “ Suala hili ni kubwa  sana,maelezo yako hapa Bungeni hayataweza kukupa haki ambayo unastahili”
     Alisema “Ushauri wangu jiandae Vizuri kusudi vyombo  vitakavyoshughulikia , vikikuita uweze kujitetea ufanye hivyo,sio humu ndani”
           
Barua hiyo ya Anna Makinda ambayo ilimjibu Prof Tibaijuka iliandikwa Novemba 28 mwaka huu ina na Kumb Na.CBC.155/188/02/16 Hata hivyo Profesa Tibaijuka hakukubaliana na majibu ya Makinda akandika tena barua nyingine siku hiyohiyo,Profesa Tibaijuka akasema “Asante kwa kujibu barua yangu.Ninakusihi sana unipe muda kuchangia kama unanitakia kheri katika maisha yangu .Dunia inasubili Kauli Yangu”

Licha ya kulalamika hivyo Spika Makinda akajibu Andishi hilo kwa kusema “Mh Prof,Tibaijuka,Bunge hili haliwezi kukusaidia.Naomba ukubali kujiandaa kwa hatua nyingine.maana wataibua hata mambo hayapo humu .Naomba unisikilize”

Habari zinasema Mbali na madai hayo Prof Tibaijuka amekuwa katika wakati mgumu na Baada ya kukatalia Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)kumlipa mshahara wa dola  marekani 19,000 (elfu kumi na tisa kwa mwezi) karibu zaidi ya Milioni 32.3 milioni mkurugenzi wa Shirika hilo Nehemia Msechu.

Bodi ya NHC iliyoidhinishwa mshahara wa dola 19,000 kwa mwezi inaongozwa na mbunge wa kuteuliwa Zakia Meghji.
Kwa sasa Msechu anaweka kibindoni dola za 11oo0 zaidi ya milioni 18 pamoja namrupumrupu mengine kedekede.

Fedha hizi ziliidhinishwa na Pro Tibaijuka na kwenda kinyume na Bodi ya Shirika hilo,Wadadisi wa Mambo wanasema kufukuzwa na kwa Waziri huyo kumeleta haheni kwa Bodi ya NHC kufanya anasa ya Fedha za Umma.

No comments: