Jamaa mmoja amefikishwa mahakamani Uingereza, kwa kuwa kitendo alichokifanya wengi hawakupendezwa nacho!
Nicholas Stewart alitumia chupa zenye nembo ya Smirnoff, Jack Daniels pamoja na Vodkaili watu wasigundue kwamba anachowauzia haikuwa whisky, chupa hizo zilijazwa mkojo.
Mshtakiwa huyo alikamatwa siku ya pili baada ya kuwauzia wateja kwa wingi mkojo huo aliokuwa amechanganya na maji ambapo alikua akitumia kipimo kile kile ambacho hutumika kupimia whisky.
Mwendesha mashtaka Victoria Cartmell kabla ya kutoa hukumu alipokea majibu kutoka kwa mkemia Mkuu ambapo yalionyesha kwamba kilichokuwa kwenye chupa sio whisky feki ila ilikuwa ni mkojo, adhabu aliyopewa haikuwa kifungo cha jela kama ambavyo wengi walitarajia, amefungiwa kufanya biashara ya kuuza vinywaji kwa miezi 2.
No comments:
Post a Comment