Thursday, 29 January 2015

HUYU NDIYE MTANGAZAJI MWENYE SHEPU KAMA KALIMATI TANZANIA

MTANGAZAJI wa kituo cha Redio Times, Hadija Shaibu ‘Dida’, juzikati aliamua kutoa siri yake ya moyoni na kuweka wazi juu ya tabia yake ya kuachika na kupata mume mpya mara kwa mara.Aliweka bayana kwamba anaachika na kupata mwanaume mpya haraka kwa sababu ana shepu ya kalimati (aina ya andazi linalonona).  

SHILOLE AMTANDIKA MAKOFI NUH MZIWANDÀ AWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE....


      

Baada ya kuzuka tetesi kuwa alimdunda vibao mchumba wake Nuh Mziwanda, Shilole amelazimika kuomba radhi.
Shilole amewaomba radhi mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram kwa kupost picha akiwa na mpenzi wake huyo na kuandika:
“Huyu hapa mjanja wangu mimi, daah nimekamatika hapa, na naamini ni mwanaume sahihi kwangu maana hawezagi kurusha hata ngumi japo namchokozaga mie mjeuri tu, mnao muhandama mme wangu mmeshindwa, kugombana ni kawaida sana kwenye mapenzi na kama nliwaudhi mashabiki wangu mnisamehe mie nampenda mme wangu.” 

Wednesday, 28 January 2015

GHANA YAICHAPA AFRICA KUSINI 2-1:YATINGA ROBO FAINALI AFCON

                             
Ghana ilitoka nyuma ikiwa kwenye hatari ya kuaga michuano na kutumia dakika 17 za mwisho kuilaza Afrika Kusini 2-1 na kutinga robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).
Katika mchezo huo uliopigwa Jumanne, mabingwa hao wa mara nne, wakaonyeshwa mlango wa kuagia mashindano baada ya mkwaju mkali wa Mandla Masango kuipatia bao Afrika Kusini kunako dakika ya 17.
Lakini Ghana wakafanikiwa kugeuza matokeo katika kipindi cha pili cha mtanange huo uliochezwa kwenye dimba la Mongomo Stadium. 

CHELSEA YAICHAPA LIVERPOOL,YATINGA FAINALI CAPITAL ONE CUP


                     

Chelsea imeifunga Liverpool 1-0 na kutinga fainali ya Capital One Cup kwa jumla ya bao 2-1 kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita.
Hata hivyo mpira huo ilibidi uchezwe kwa dakika 120 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 za kawaida bila kufungana.
Dakika ya 4 tu ya dakika 30 za ‘Extra Time’ beki Branislav Ivanovic akaifungia Chelsea bao pekee baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya mpira wa adhabu uliopigwa na Willian.  

HII NDIO ORODHA YA PASSWORD ZILIZOVUJA ZAIDI NA ZILIZITUMIWA NA WEZI WENGI WA MITANDAO 2014,TAZAMA KAMA YAKO IPO..


Hivi karibuni tumesikia watu wengi wakiwemo wasanii wakilamika juu ya account zao pamoja na simu kuvamiwa na wezi wa mitandaoni, watafiti wanasema matumizi ya password dhaifu pia huchangia account hizo kuvamiwa, au wengine kutumia password moja kwenye account zaidi ya moja ikiwemo email, simu na mitandao ya kijamii.

Sunday, 25 January 2015

MREMBO MTANZANIA ALIYEJIUNGA NA FREEMASON AJITOKEZA AELEZA MAZITO

  
Happiness Wilfred Nassari (27), ameibuka na kudai kuwa amekuwa akisali bila nguo kwenye ibada ya imani ya Freemason inayosifika kwa ushirikina. 

Katika mahojiano yaliyofanyika hivi karibuni Bamaga, Mwenge jijini Dar, Happiness alisema kuwa, alianza kuingia kwenye imani hiyo kwa kwa kupitia kaka yake mmoja (jina tunalo) ambaye ni tajiri wa kupindukia kutokana na kuwa mshiriki wa Freemason.

“Nilipojiunga ilikuwa si kwa matakwa yangu, kwani nilianza kwa kupata matatizo ya kuumwa magonjwa ya ajabuajabu, ikiwemo kutokwa na wadudu usoni kiasi cha kunitoa vidonda,” alisema mrembo huyo huku akionesha makovu ya vidonda hivyo.

PROF.MUHONGO AJIUZURU ASISITIZA YEYE NI MSAFI,ANA HESHIMIKA NA SIO MWIZI WA MABILIONI YA ESCROW

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano aliouitisha jana ofisini kwake, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake wa Uwaziri baada ya kutuhumiwa kuwa yeye ndiye tatizo linaloendeleza malumbano baina ya Serikali na Bunge kuhusu fedha za akaunti ya Tegera Escrow. 

TAZAMA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI

Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo jana mchana, Rais Jakaya Kikwete ametangaza marekebisho ya Baraza lake la Mawaziri.

Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi ya Rais,  Ombeni Sefue alitaja mawaziri hao wapya ambao wameapishwa jana jioni na wizara zao kwenye mabano kuwa ni: George Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).