Wednesday, 28 January 2015

HII NDIO ORODHA YA PASSWORD ZILIZOVUJA ZAIDI NA ZILIZITUMIWA NA WEZI WENGI WA MITANDAO 2014,TAZAMA KAMA YAKO IPO..


Hivi karibuni tumesikia watu wengi wakiwemo wasanii wakilamika juu ya account zao pamoja na simu kuvamiwa na wezi wa mitandaoni, watafiti wanasema matumizi ya password dhaifu pia huchangia account hizo kuvamiwa, au wengine kutumia password moja kwenye account zaidi ya moja ikiwemo email, simu na mitandao ya kijamii.


Utafiti uliofanywa na  kampuni ya SplashData, Marekani umeonyesha kuwa password milioni 3.3 zilizotumika mwaka 2014 katika maeneo ya Amerika ya Kaskazini na Ulaya Magharibi zilivuja huku majina kama Michael, Thomas, Andrew na Daniel yakionekana kuwa majina yanayotumiwa sana kwenye password.
Takwimu hiyo imeonyesha kuwa password nyingi ambazo zinatumika zimekuwa ni rahisi sana kiasi kwamba zinawapa urahisi hackers kuzitabiria na kuweza kuvamia account hizo kirahisi na kushauriwa password nzuri ni ya kuchanganya namba na tarakimu.
Utafiti huo umetoa password 25 zilizotumiwa na watu wengi duniani kwa mwaka 2014, ambazo ni 2.2% ya password zote.
Hii ni list ya password hizo 25 ambazo zimetumika zaidi 2014.
:: 123456
:: password
:: 12345
:: 12345678
:: qwerty
:: 1234567890
:: baseball
:: dragon
:: football
:: 1234567
:: monkey
:: letmein
:: abc123
:: 111111
:: mustang
:: access
:: shadow
:: master
:: michael
:: superman
:: 696969
:: 123123
:: batman
:: trustno1

No comments: