Wednesday, 26 November 2014
ISOME RIPOTI YA ESCROW NA MAPENDEKEZO YAKE
Taarifa hii ina sehemu mbili na itasomwa na mwenyekiti na makamu mwenyekiti na anaanza kuisoma ripoti, Migogoro ilitakiwa iishe kwanza ili pesa zililipwe 2014 March kamati ya PAC ilikutana na BoT ili kujadili pesa zilizo kwenye walisema pesa zimeshatolewa na zimeshalipwa IPTL, kamati iliomba ofisi ya CAG kufanya ukaguzi.
Majadiliano bungeni: Waheshimiwa wabunge wamejadiliana kwa namna tofauti, kundi la kwanza wamekuwa wakisema fedha hizo ni za umma na kundi la pili wamekuwa wakisema ni fedha za IPTL na zilikuwa sawa kulipwa IPTL.
Anawataja wanakamati waliochambua waliochambua ripoti, kwanza kamati ilifanya uchambuzi wa mkataba wa kufua umeme. Serikali 1995 iliingia mkataba wa kuuziana umeme kwa miaka 20 lakini mkataba wa awali ni miaka 15
Mwaka 1997 ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme ulikamilika. Hata hivyo, TANESCO ilibaini kwamba gharama za ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme ambazo IPTL iliwasilisha kwake zilikuwa kubwa tofauti na makubaliano ya kwenye Mkataba. IPTL ilikuwa imefunga injini zenye msukumo wa kati ( medium speed) zenye gharama ndogo na uwezo mdogo badala ya injini za msukumo mdogo ( low speed) zenye nguvu kubwa na bei kubwa. Wakati huo huo IPTL waliendelea kutoza kiasi kikubwa cha fedha kinacholingana na gharama ya ufungaji wa mtambo wenye msukumo mdogo ( low speed) .
Kutokana na IPTL kukiuka makubaliano ya Mkataba kama ilivyoelezwa hapo juu, mwaka 1998 TANESCO ilifungua Shauri Na. ARB/98/8 katika Baraza la Kimataifa la Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (The International Centre for Settlement of Investiment Disputes - ICSID) kupinga ukiukwaji huo. Katika Hukumu iliyotolewa na ICSID, IPTL iliagizwa kupunguza gharama za uwekezaji kutoka USD 163.531 milioni hadi USD 127. 201 milioni kwa mwezi.
Ujenzi wa Mtambo ulikamilika mwaka 1997 lakini uzalishaji na uuzaji wa umeme ulianza mwaka 2002. Kwa mujibu wa makubaliano ya kuzalisha umeme, TANESCO ina wajibu wa kulipia gharama za uwekezaji ( capacity charges ) kwa wastani wa USD 2.6 milioni kila mwezi.
Kwa mujibu wa uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, imebainika kuwa chanzo cha mgogoro kati ya TANESCO na IPTL ambacho ndio kilisababisha kufunguliwa kwa Akaunti ya Tegeta ESCROW, ni taarifa ziliyoifikia Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO mnamo tarehe 01 Aprili, 2004. Kaika Taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine walifahamishwa na mmoja wa wanahisa wa IPTL, Kampuni ya VIP Engineering, kuwa kuna viashiria kuwa TANESCO wanailipa IPTL capacity charges kubwa.
Baada ya kupokea taarifa hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO iliiteua Kampuni ya Uwakili ya Mkono ili kufuatilia madai hayo na kutoa ushauri kwa Bodi
Kwa kuzingatia ushauri wa Kampuni ya Uwakili ya Mkono, Menejimenti ya TANESCO kupitia barua namba DMDF&CS/02/05, tarehe 17 Juni, 2004 walitoa Notisi kwa IPTL ya kutoendelea walichokuwa kulipa capacity charges kwa sababu kiwango wanatozwa ni kikubwa kuliko inavyostahili.
Pamoja na kutoa Notisi hii Kamati imebaini kuwa Bodi na Menejimenti ya TANESCO kwa nyakati tofauti walizitaarifu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Nishati na Madini, na Msajili wa Hazina kuomba zichukue hatua stahiki kutatua mgogoro uliokuwa unaendelea. Kamati ilifanikiwa kuona barua Na. NEM/740/05 ya tarehe 6 Desemba, 2005 kutoka kwa Kampuni ya Uwakili ya Mkono kwenda kwa aliy
ALICHOANDIKA Dr SLAA ON Twitter KUHUSU SAKATA LA ESCROW
-‘…Tulisema hili la Escrow mapema. Akaunti nyingi zilizopokea hela zilikuwa ni mpya, nyingine hazikuwa hata na vitabu vya hundi. Hatuliachi….”
-“… Ni jambo la kusikitisha sana kuona hata benki zinazomilikiwa na madhehebu ya dini sasa zimekuwa sehemu ya kusambaza fedha zilizoibwa…’.
-‘…Fisadi anapoachia ngazi bila kufikishwa mbele ya sheria ni sawa na kupewa mapumziko kwenda kutumia alichofisadi. Kuachia ngazi tu haitoshi…’.
SASA NI ZAMU YA WAKAZI WA BAGAMOYO KUPONDA MARAHA BAHARINI
“Kivuko hiki ndicho bora kuliko vyote kati ya 27 tulivyonavyo nchi nzima. Kitabeba watu zaidi ya 500 ukijumlisha na wengine watakaokuwa wamesimama”
Usafiri wa majini una raha yake, hasa ikiwa chombo unachotumia ni imara na chenye usalama usiotiliwa shaka.
Wasafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar ni mashuhuda wa baadhi ya vyombo vya majini vyenye mvuto wa aina yake. Ukiwa katika vyombo hivi utafurahia mwonekano wake, mwendo na sifa nyinginezo.
Kwa watu wengi hasa wanaotumia vyombo hivi, usafiri katika maeneo hayo ni zaidi ya safari. Ni utalii wa aina yake.
Ukiondoa raha ya wasafiri wa Dar es Salaam na Zanzibar, sasa ni zamu ya wakazi wa Dar es Salaam na Bagamoyo. Kwa wasiotaka usafiri wa barabara, Serikali imewaletea usafiri wa majini. Kivuko cha Mv Dar es Salaam, kimewasili nchini tayari kutoa huduma ya usafiri kati ya maeneo hayo.
Pamoja na kivuko hicho kuelezwa kuwa kitasaidia kupunguza msongamano wa magari, matumizi yake yanaweza pia kuchukua sura ya utalii
“Hiki kivuko kitakuwa na matumizi mengi, wengine watapenda kufungia ndoa humo, wengine watakuwa wakitalii. Naomba Watanzania wakitunze ili kidumu,” anasema Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli.
Mv Dar es Salaam
Katika hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2013/14, Dk Magufuli alitaja miradi mbalimbali itakayosaidia kupunguza foleni katika jiji hili. Miongoni mwa miradi hiyo ilikuwa ni ujenzi wa kivuko kitakachofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo.
Novemba 17, mwaka huu kivuko hicho kiliwasili nchini kutoka Bangladesh baada ya safari ya siku 14 kikiwa chini ya usimamizi wa mkandarasi, Kampuni ya Johs Graham-Hanssen M/S ya Denmark.
Dk Magufuli anasema kivuko hicho chenye thamani ya Sh7.9 bilioni, kina mwendo wa kasi zaidi kuliko kivuko chochote nchini na kina uwezo wa kubeba watu 300 waliokaa, huku wengine wakisimama.
Anasema kivuko hicho pamoja na miradi mingine kama vile ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka (BRT), barabara za pembeni na barabara za juu, kitasaidia kupunguza msongamano wa magari ambao umekuwa sugu kwa sasa.
Chanzo: Mwananchi
PAPA FRANCIS ATAKA MAJADILIANO NA WAPIGANAJI WA DOLA YA KIISLAM
Baba mtakatifu Francis ametaka milango ya majadiliano na kundi la wanamgambo wa dola ya kiislam iwe wazi ,ingawa hali ni mbaya na ya kutatiza katika maeneo wanako tekeleza mashambulio yao.
Papa Francis ameyasema hayo wakati akirejea mjini Rome, Italia,baada ya kulitembelea bunge la muungano wa jumuiya ya Ulaya lilifanyika katika mji wa Strasbourg, Papa pia amesisitiza makubaliano ya kimataifa kutokomeza ugaidi yalikuwa muhimu.na hakuna ulazima wa nchi kupigana na ugaidi ikiwa peke yake nguvu ya pamoja ni muhimu sana.
Akilihutubia bunge hilo ,alishusha mvua za lawama kwa muungano huo kuwa una hatia kwa kuweka sheria zilizokuwa kali na za kuumiza, hasa katika suala la wahamiaji na kuonya kuwa Mediterranean isifanywe kuwa kaburi la wahamiaji wanaosafiri kwa boti kutokea upande wa kaskazini mwa Africa
UEFA: CHELSEA NOUUUUMAAAA....BAYERN YAGONGWA 3...
Usiku wa kuamkia leo kindumbwe ndumbwe cha michuano ya Klabu Bigwa barani Ulaya kiliendelea na kushuhudia Chelsea ikitoa kipigo cha mbwa mwizi mbele ya mashabiki wa Schalke 04 ya Ujuremani pale ilipoishindilia magoli 5 bila majibu.
Manchester City ya England nao wakawabamiza wababe wengine wa Ujerumani Bayern Munich kwa kwa kuwafunga magoli 3 - 2 na kufufua matumaini ya kusonga mbele katika michuano hiyo huku magoli yote matatu ya Man City yakitiwa kimiani Sergio Aguero.
Katika mechi nyingine Paris St. Germain ya Ufaransa waliwashikisha adabu Ajax ya Uholanzi kwa kuifunga magoli 3 - 1 huku Becelona kwa upande mwingine wakiisasambua Apoel Nicosia ya Syprus kwa kuishushia kichapo cha magoli 4 kwa yai.
CSKA Moscow ya Urusi na AC Roma zikatoka suluhu ya goli moja 1 - 1
Burudani hiyo itaendelea leo ambapo Liverpool ya England baada ya kufanya vibaya katika mechi zilizotangulia leo wanajaribu bahati yao wakiwa ugenini dhidi Ludogorets ya Bulgaria.
Arsenal nao watawakaribisha Borusia Dortmud ya Ujerumani huku vita vingine vikiwa ni kati ya FC Basel ya Uswis watakaopopepetana na Real Madrid. Malmo FF ya Sweden watakuwa wenyeji wa Juventus ya Italia
OBAMA AMPA POLE JK
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa Jumatatu, Novemba 24, 2014 amepokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Marekani Mheshimiwa Barak Obama.
Katika salamu zake Rais Obama ameelezea kufurahishwa na taarifa kwamba Rais Kikwete anaendelea vyema kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji kwa mafanikio na kuondoa tatizo la tezi dume alilokuwa nalo.
Rais Obama amesema katika salamu hizo kuwa alipata heshima kufanya ziara rasmi nchini Tanzania mwaka 2013, na pia kumualika Rais Kikwete kwenye mkutano wa Marekani na viongozi wa Afrika mwaka huu.
“Nakutakia kasi ya kupona kabisa na nataraji kuendelea kufanya kazi nawe katika masuala tuliyokubaliana ya kipaumbele”, amesema Rais Obama kwenye salamu zake hizo.
Rais Kikwete amekabidhiwa salamu hizo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula, aliyekuwa ameongozana na maafisa waandamizi wa ubalozi waliofika Baltimore kumjulia hali.
Mhe. Mulamula amesema salamu kutoka sehemu mbalimbali duniani zimekuwa zikimiminika ubalozini kwa njia mbalimbali.
Taratibu za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zilikamilika Jumatatu, Novemba 24, 2014 asubuhi baada ya madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, kumfanyia hatua ya mwisho ya tiba.
Rais Kikwete ameendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.
Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.
Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.
Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
25 Novemba,2014
BOKO HARAM WAENDELEA KUFANYA YAO....SASA WATEKA MJI MWINGINEMWINGINE WA KASKAZIN
Duru za habari nchini Nigeria, zimetangaza kuwa, wanamgambo wa kundi la kigaidi na kitakfiri wa Boko Haram wameudhibiti mji mwengine wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Hayo yamethibitishwa leo na kiongozi mmoja wa serikali katika bunge la seneti nchini Nigeria ambaye ni mkazi wa jimbo la Borno na kuongeza kuwa, wanachama wa kundi hilo lenye uelewa potofu kuhusu mafundisho ya Uislamu, wameudhibiti mji wa mpakani wa Damasak. Seneta huyo ameongeza kuwa, hivi sasa mji huo umetwaliwa na kundi hilo na kwamba, raia na askari wamelazimika kukimbia kuokoa maisha yao. Inaelezwa kuwa, awali wanamgambo wa kundi hilo waliokuwa wameficha silaha zao katika magari aina ya malori, walipeleka magari hayo katika soko la mji huo, na kuanza kuwamiminia risasi wafanyabiashara na raia wa kawaida, ambapo makumi ya watu waliuawa. Seneta huyo ameongeza kuwa, baada ya wanachama wa kundi hilo la Boko Haram kuudhibiti mji huo, walianza kubomoa na kuharibu nyumba nyingi ikiwemo hospitali na kwamba hadi sasa makumi ya wasichana na watoto wadogo wametekwa na magaidi hao.
TIGO TANZANIA YAGĂ€WA MABILIONI KWA WATEJA WAKE
Tigo imetangaza jana kwamba imetoa malipo yake ya kwanza ya kila robo mwaka ya kiasi cha shilingi bilioni 3 (dola milioni 1.8) kwa wateja wake wa Tigo Pesa. Mgao huu ni wa kwanza kati ya awamu nne za malipo zinazotarajiwa kufanyika kila mwaka.
Malipo haya yanafanyka miezi mitatu baada ya kampuni hiyo kulipa kiasi cha shilingi bilioni 14.25 (dola milioni 8.64) ambacho kilikuwa kimelimbikizwa katika mfuko wa fedha ya akaunti ya Tigo Pesa, malipo yaliyoifanya Tigo kuwa kampuni ya simu ya kwanza duniani kuwagawia faida watumiaji wake wa huduma ya fedha kwa simu za mkononi. Tigo Pesa ina jumla ya watumiaji milioni 3.6.
Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez alisema, “Hii duru ya pili ya kutoa gawio ni udhihirisho tosha wa muendelezo wa kampuni yetu katika kuwanufaisha wateja na kuboresha maisha ya Watanzania. Malipo haya yanaenda kwa kila mtumiaji wa Tigo pesa wakiwemo mawakala wakuu, mawakala wa reja reja na watumiaji wa kawaida wa huduma hii. ”
“Gawio la kwanza lilikuwa kubwa zaidi kwa sababu faida ilimbikizwa kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu na nusu ikilinganishwa na malipo haya ya pili ambayo yanatokana na malimbikizo ya faida ya fedha zilizohifadhiwa katika mifuko ya benki za kibiashara kwa muda wa miezi mitatu t kutoka Julai hadi Septemba 2014,” alisema Meneja Mkuu huyo.
Gutierrez alieleza kwamba, kama ilivyokuwa hapo awali, malipo wanayopata wateja awamu hii yanatokana na salio lao la kila siku kwenye akaunti zao za Tigo Pesa. Hii ni kwa wote; mawakala wakuu, mawakala wa reja reja na watumiaji wa kawaida.
Mgao unaofuata wa mwezi Oktoba mpaka Desemba 2014 utalipwa mwezi Februari 2015.
Subscribe to:
Posts (Atom)