Sunday 18 January 2015

MCHUNGAJI MTIKILA AMSHTAKI ASKOFU MOKIWA BAADA YA KUMSHIKA MAKALIO ADAI FIDIA YA BILIONI MOJA


Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumshitaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Dk. Valentino Mokiwa.
Msingi wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana walipokutana maeneo ya Ilala, kimemdhalilisha.
Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe. 

DIAMOND NA KIBA WAKUTANA UKUMBINI,WACHUNIANA....

     
Kama ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi utakuwa utakuwa unakosea na kujidanganya vibaya mnooooo.....Bifu bado lipo na hii imegundulika baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana. 

LULU: SICHANGANYI MADAWA KAMA WENGINE,NITABAKI KUWA MUIGIZA


MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema katika maisha yake ya sanaa hataweza kuchanganya madawa kufanya kazi nyingine mbali na kuigiza kama ambavyo wasanii wengine wanafanya. 

AMINI USIAMINI,MJI WA DUBAI UNAONGOZA KWA UAMINIFU SOMA TAARIFA HII...

Dubai imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za jamii kwa pochi iliyoangushwa mtaani,na mara ikarejeshwa kwa mhusika mara moja. 

Katika utafiti uliofanywa na mtengeneza Filamu mwenye asili ya Uingereza katika mitaa ya Dubai, alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha kwa makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi hiyo kwa mmiliki wake. 

SALUNI INAYOTOA HUDUMA YA NGONO YAGUNDULIKA KINONDONI,WADADA WA KISOMALI NDIO WAHUDUMU,BEI NI TSHS 60,000 KWA TENDO..

 
Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya watu kubuni mtindo mpya wa kujipatia fedha kwa kujihusisha na biashara haramu ya ngono katika maeneo yanayotambulika kufanya shughuli nyingine halali.

Saturday 17 January 2015

WANAFUNZI 84 UDOM WAFIKISHWA MAHAKAMANI...


Wanafunzi 84 wa programu maalum ya stashahada ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma(udom) waliofanya mgomo na kuandamana kushinikiza kulipwa madai yao, juzi wamepandishwa kizimbani kwa kosa la kukusanyika bila kibali maalum.

TANZANIA SIO NCHI MASKINI...VIGOGO BANDARINI WANALIPWA POSHO LAKI 5 KWA SIKU TANGU 2011

Wakati Msajili wa Hazina amebariki posho mpya za safari za ndani kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) kuwa Sh 500,000 kwa siku kuanzia Januari 2, mwaka huu, imebainika kuwa walishaanza kulipana hivyo tangu mwaka 2011.

WATUHUMIWA WENGINE 3 WA SAKATA LA ESCROW WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Maafisa watatu mmoja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Mapato (TRA) pamoja na wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) leo wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusiana na  kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.