Saturday 20 December 2014

PLUIJM ASAINI MWAKA MMOJA NA NUSU KUINOA YANGA


       Kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van Der Pluijm.
WAKATI kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van Der Pluijm akisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuinoa Yanga jana, Mbrazili aliyefungashiwa virago, Marcio Maximo juzi usiku alikabidhiwa kitita chake cha dola 12,000 (zaidi ya Sh milioni 20) na kumalizana kabisa na Yanga.
Pluijm aliyetua kuifundisha timu hiyo Jumatatu ya wiki iliyopita, amesaini mkataba huo baada ya Yanga kumalizana na Maximo ambaye wamempa mshahara wake wa mwezi mmoja kama walivyokubaliana kimkataba. 

BAADA YA DIAMOND KUDAI MIMBA ALIZOMPA PENNY ZILIHABIKA KIUTATA! ZILIPENDWA HUYO AFUNGUKA KIIVI!


    
 

FLORA MBASHA AWASILISHA MAHAKAMANI DAI LA TALAKA OMBI LA MGAO WA MALI NA MTOTO

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania,Flora Mbasha, amekwenda katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar-es-Salaam, akiomba kuvunjwa kwa ndoa yake na mumewe Emanuel Mbasha.
Flora amefungua kesi ya madai namba 64 ya mwaka huu kesi ambayo inasikilizwa na hakimu Maxi, Devota Kisoka. 

WOLPER NA KING MAJUTO NDANI YA BONGE MOJA LA MOVIE


      
Tukiwa unaelekea ukingoni mwa mwaka 2014 , Waigizaji Jackline Masawe “Wolper”na King Majuto wameonekana wakiwa mzigoni kutengeneza kitu kipya. Mwanadada Wolper aliidondosha picha hii na kuandika “New Movie with majuto dady”

MPAMBE WA MGOMBEA URAIS 2015 AFUMANIWA AVISHWA SHANGA...


        
JAMAA anayedaiwa kwamba ni mpambe mkubwa wa mmoja wa wagombea urais mwakani ambaye ni fundi wa kufunga madishi, mkazi wa Magomeni-Makanya jijini Dar es Salaam, almaarufu Mgosingwa, amejikuta akivishwa shanga baada ya kunaswa na mke wa mtu chumbani kwake.
    

Friday 19 December 2014

MAXIMO OOOUUUUTTTT PRUIJM NA MKWASA WARUDI KUINOA YANGA..!!!....

Baada ya kuwepo kwa taarifa zisizothibitishwa rasmi za kufukuzwa kazi kwa kocha mkuu wa timu ya Dar es salaam young African Mbrazil Marcio Maximo, hatimae hii leo uongozi wa timu hiyo umemtangaza rasmi Mdachi Hans Van Der Pruijm kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

MOVIES ZA KIBONGO KUSHUKA BEI IFIKAPO MWAKANI



Baadhi ya waigizaji na wadau wanaofanya kazi na kampuni ya Steps Entertainment , leo asubuhi walitambulisha bei mpya na muonekano mpya wa DVD covers za filamu zao kwenye ukumbi wa habari maelelzo.

JOKATE NEXT LEVEL...ASAINI MKATABA WA BILIONI 8.5 NA KAMPUNI YA KICHINA KUMTENGENENZEA BIDHAA ZAKE ZA KIDOTI...


                                        

Mrembo Jokate Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya Kichina,  Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.