Friday 19 December 2014

VAN VICKER AWASHANGAA WABONGO

                                             
Mwigizaji na mwongozaji wa filamu wa nchini Ghana, Van Vicker ameshangazwa na vyombo vya habari za udaku za hapa Bongo, kwa kile ambacho kimelipotiwa kuhusu yeye na muigizaji Wema Sepetu.
Kwenye blogs na magazeti mbalimbali ya udaku hapa Bongo zilijaa habari za kuwa Wema na Van Vicker mbali kucheza movie kuna mambo mambo walifanya eti kwa sababu tu Wema ameachana na aliekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz na hivyo alitaka kumrusha roho, kitu ambacho hakina ukweli wowote. 

Thursday 18 December 2014

WAZIRI ANNA TIBAIJUKA ASEMA AKIJIUZURU RAIS ATAMSHANGAA...

 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka amegoma kujiuzulu kwakuwa haoni sababu ya kufanya hivyo...  

KANISA LACHAGUA ASKOFU MWANAMKE KWA MARA YA KWANZA


               
Kanisa la Uingereza limemchagua askofu wa kwanza mwanamke.Mchungaji Libby Lane atakuwa askofu wa Stockport mnamo mwezi January ,na kumaliza ukiritimba wa wanaume kuwa maaskofu katika kanisa hilo.Amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo.Kanisa la Uingereza liliwachagua wanawake mara ya kwanza kama makuhani mnamo mwaka 1994.Wanawake tayari wameruhusiwa kuwa maaskofu katika maeneo mengine ya jamii ya kianglikana ,ikiwemo Marekani na kusini mwa Afrika.

CHANZO: BBC SSWAHILI

Mh.RAIS AKIRI IDADI KUBWA YA WANACHUO UDOM KUWA NI MAKAHABA...

 

DIAMOND AANIKA SABABU ZA KUWAACHA PENNY,JOKATE NA WEMA..


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa katika pozi.
KWA mara ya kwanza supastaa ndani na nje ya Bongo kutoka muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewafungukia waliowahi kuwa wapenzi wake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Wema Sepetu ‘Madam’ na Penniel Mungilwa ‘Penny’ kuwa waligoma kumzalia mtoto.  

WEMA SEPETU AMCHANA KWEUPEEEE ZAMARADI MKETEMA WA CLOUDS ..


Mara baada ya mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha maswala ya filamu nchini cha TAKE ONE, Zamaradi Mtetema kuweka bandiko mtandaoni, akiwatata mashabiki na wapenzi wake, wataje mambo matano ambayo niyaukweli kuhusu yeye Zamaradi kwa jinsi wanavyomuona na atatoa zawadi kwa yule atakae patia.  Madam Wema Sepetu alikuwa ni mmoja kati ya watu waliojitokeza kwa kumwambia ukweli bila kumficha wala kusita na kutoa 5 facts za ukweli kabisa... 

HAYA NDIO MAJANGA YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


HAYA MAJANGA! Wakati vuguvugu la uchaguzi wa serikali za mitaa likiwa bichi, baadhi ya sehemu zikiwa zinasubiri zoezi hilo kutokana na sababu tofauti, matukio mbalimbali, yakiwemo ya kusikitisha, yameripotiwa. 
 Wananchi wakiutoa mwili wa marehemu Bandoma Mabele (58) majini.

Huku washindi wa nafasi mbalimbali zilizokuwa zikigombewa wakisheherekea kwa namna ya aina yake, katika Kijiji cha Mwagika, Sengerema mkoani Mwanza, kulitokea msiba wa kusikitisha, baada ya mgombea wa nafasi ya Uenyekiti, aliyetambulika kwa jina la Bandoma Mabele (58) kufariki dunia kufuatia kuzama ndani ya maji ya ziwa Victoria. 

BI.CHEKA ANAHITAJI MSAADA WA HARAKA


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Bi Cheka hivi sasa ni mgonjwa. Anahitaji matibabu na huduma muhimu kutokana na umri wake mkubwa 
(ana miaka 55).
Hali yake kimaisha ni mbaya, kwani anaishi katika kibanda cha udongo, yeye na wajukuu zake. Global Publishers inaendesha harambee hii ili aweze angalau kujenga kibanda cha bati na kupata matibabu. 

Mchangie chochote ulichonacho, iwe 500, 1000, 5000 au zaidi kupitia namba 0654 880 707. Kitakachopatikana mtatangaziwa. Kutoa ni Moyo!