Thursday 4 December 2014

UKAWA WAANZA KUSALITIANA ARUSHA


VYAMA vinne vya upinzani vilivyoungana na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vimeshindwa kuachiana nafasi za uongozi mkoani Arusha, katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14.

Mh.ZITTO KABWE APATA MCHUMBA


MBUNGE Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amemtambulisha mchumba wake mpya anayetarajia kufunga nae pingu za maisha hivi karibuni. 

188 WAHUKUMIWA KIFO NCHINI MISRI


Mahakama moja ya Misri imewahukumu kifo wafuasi 188 wa harakati ya Ikhwanul Muslimin kwa madai ya kuhusika kwenye shambulio lililotokea mwaka 2013 katika kituo cha polisi mjini Cairo. Hukumu hiyo ilitangazwa hapo jana ambapo watu hao wanadaiwa kushambulia na kuua askari kadhaa wa usalama.  Wakati huo huo maelfu ya wananchi wa Misri wameandamana nchini humo kupinga uamuzi wa mahakama wa kumfutia mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili dikteta wa zamani wa nchi nchi hiyo Hosni Mubarak.

Waandamanaji hao huku wakitoa nara za kupinga serikali na kulaani utawala wa kijeshi wa Misri, wamesema kuwa hawatosalimu amri hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa. Polisi ya Misri imefunga barabara zote zinazoelekea katika Meidani maarufu ya mjini Cairo ambako hukusanyika waandamanaji, baada ya kuanza wimbi jipya la malalamiko ya wananchi ya kupinga kufutiwa mashtaka Hosni Mubarak.  

SIRI YA MTUNGI SEASON 2 HIYOOOOOOOOO KUANZATAREHE 7 NDANI YA TBC1..


Akizungumza jijini jana, Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka  Shirika Lisilo la Kiserikali la  Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.

KOREA KASKAZINI YAAMURU RAIA WENYE JINA KAMA LA RAIS KUBADILI MAJINA YAO MARA MOJA..


   
Rais Kim Jong Un

DAKTARI ATUMIA PAMPU YA BAISKELI KUFANYA UPASUAJI


AFCON 2015: MAKUNDI YATAJWA


Upangaji wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015 yamefanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo. 

Wednesday 3 December 2014

SPIKA: MSIOE WANAWAKE WALIOKEKETWA...


Spika wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amewashauri wanaume kutowaoa wanawake waliokeketwa akiwataja kuwa mzigo ambao hauwezi kuijenga jamii.