Monday, 29 December 2014

MC ZIPOMPA ATAPELIWA NA STARA THOMAS,AAHIDI KUMVURUGA VURUGA...

Glads Chiduo ‘MC Zipompa’. 
MSHEREHESHAJI maarufu Bongo, Glads Chiduo ‘MC Zipompa’ ameibuka na kusema kwamba endapo staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Stara Thomas hatamlipa fedha zake, atamvuruga kwani amemvumilia vya kutosha na ameenda kinyume na makubaliano yao.  
Akizungumza nasi wikiendi iliyopita jijini Dar, MC Zipompa alisema: “Nilimpa muziki akafanyie shughuli yake kwenye Ukumbi wa Karimjee (Dar), akanilipa laki moja na nusu ikabaki elfu hamsini, akaniahidi angelipa siku inayofuata lakini kila nikimpigia simu hapokei na nilipomtumia SMS alijibu yuko Arusha kwenye kikao.”
Staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Stara Thomas. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, mwanahabari wetu alimtafuta Stara ambaye alikiri kudaiwa kiasi hicho cha fedha na kusema kuwa simu yake iliharibika ndiyo maana alishindwa kuwasiliana na Zipompa ila atamlipa. 
“Mimi si wa kumtapeli Zipompa hiyo fedha ni ndogo sana kwangu,” alisema Stara

No comments: