Monday, 29 December 2014

100% ROSE MUHANDO ASUMBULIWA NA PEPO CHAFU LA UTAPELI...SAFARI HII AMTAPELI MDAU WAKE WA KARIBU SANA...


                             

Nyota wa muziki wa injili nchini, Rose Athuman Muhando.

LILE jinamizi la kupokea fedha kwa ajili ya kushiriki tamasha la kuimba nyimbo za Injili kisha kutotokea siku ya tukio linazidi kumwandama nyota wa muziki huo nchini, Rose Athuman Muhando, safari hii akidaiwa kumliza tena mtu, Ijumaa Wikienda lina kesi hiyo mkononi. 

Kwa mujibu wa chanzo makini cha ndani, safari hii ameendelea kupokea fedha kutoka kwa mshirika wake kwenye mambo ya Injili, Alex Msama kwa makubaliano ya kushiriki Tamasha la Krismasi kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa lakini siku ya tukio, Ijumaa iliyopita, mwanadada huyo hakutokea!
Chanzo kilisema: “Hivi jamani mnajua kuwa, Rose Mhando amemliza tena Alex Msama? Amepokea fedha kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Krismasi, Iringa lakini pamoja na kupokea fedha hizo ameingia mitini.....

No comments: